Friday, August 19, 2011

KANALI DAKTA JANGA AKANUSHA HABARI ZA KUAWAASKARI WAKE AMEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 KWA KOSA LA UBAKAJI


Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) Mkoa wa Mbeya Kanali dakta Janga amekanusha habari zilizoandikwa na gazeti la Serikali kuwa askari wake amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la ubakaji.

Gazeti hilo liliandika habari kuwa askari JWTZ, Kambi ya Mbalizi, Mbeya, Saje Michael mwenye umri wa miaka 44 amehukumiwa kifungo cha miaka 30 na kulipa faini ya milioni moja baada ya kupatikana na hatia ya kumnajisi mtoto wa mtalaka wake mwenye umri wa miaka mitatu.

Alihukuhumiwa kifungo hicho katika Mahakama ya Hakimu Mkoa ya Mkoa wa Mbeya ambako Hakimu Mkazi Maria Amosy, alimtia hatiani baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka.

Kanali Janga amesema kuwa Saje Michael hakuwa mwanajeshi ila baba yake ndiye aliyekuwa mwanajeshi hata hivyo amekwisha staafu miaka mingi iliyopita na Sanje alikuwa akihisi uraiani na sio kambini.

Habari za mahakama zinadai kuwa mshitakiwa alimnajisi mtoto huyo walipopitia nyumbani kwake wakati akienda kwa bibi yao mzaa mama anayeishi Mbalizi na kwamba mtuhumiwa alikuwa akihishi mtaa wa Mtakuja Halmashauri ya wilaya ya Mbeya
.

No comments: