WAKATI taifa likiwa katika maombolezo ya msiba mkubwa wa ajali ya Meli ya MV Spice Islanders,watu wanne jana wamenusurika kupoteza maisha, baada ya ndege ndogo waliyokuwa wakisafiria kutoka Mbeya kwenda Jijini Dar es salaam kuanguka.
Kwa mujibu wa taarifa za awali zilizopatikana muda mfupi baada ya Ndege hiyo ndogo yenye namba za usajiri 9J-BIO SESINA 206 kuanguka zinadai kuwa ilikuwa na watu wane,wakiwemo wawekezaji wa kampuni ya Export Trading Company, ambayo inaendesha Shamba la Kapunga lililopo wilayani Mbarali mkoani hapa.
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa tatu asubuhi baada ya ndege hiyo kuanguka katika katika eneo la Chuo cha kilimo na Utafiti Uyole jijini hapa muda mfupi baada ya kuruka kutoka katika uwanja wa ndege wa Jijini hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio, Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Anacletus Malindisa alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana ambapo rubani wa ndege hiyo Jver Waak alisema chanzo ni hitilafu iliyotokea katika injini kabla ya kuanguka kisha kupoteza mwelekeo na kuanguka.
Aliwataja watu walionusurika katika ajali hiyo ni pamoja na rubani wa ndege hiyo, Jver Waak (49), raia wa Afrika kusini, Balozi Mohamed Ramia (64) ,Christian Mmasi (30) ambaye ni ofisa utawala wa shamba la Kapunga, pamoja na Sunil Taril (50) ,Meneja wa mashamba hayo ya Kapunga.
Hata hivyo Kamanda Malindisa alisema kuwa katika ajali hiyo, hakuna aliyepata majeraha yeyote wala kupoteza maisha zaidi ya baadhi yao kupata mshtuko..
Katika eneo hilo la tukio kumekuwa na mfululizo wa ajali za ndege ndogo ambapo miezi saba iliyopita ndege ndogo ilianguka na kusababisha kifo cha mwanafunzi wa shule ya sekondari Swilla iliyopo Mbeya Vijijini mkoani hapa.
Tukio la kuanguka kwa ndege hiyo limekuwa ni mfululizo wa matukio hayo mkoani hapa ambapo miezi saba iliyopita ndege ndogo kama hiyo ilianguka na kusababisha kifo cha mtu mmoja Godfrey Mpoli,ambaye alikuwa alifia papo hapo na wengine wengine watatu kujeruhiwa vibaya.
No comments:
Post a Comment