Na Rodrick Mushi,Rombo.
Malalamiko kwa baadhi ya viongozi ambao wamekuwa siyo wadilifu kwa kushiriki katika vitendo mbalimbali vya kuomba na kupokea rushwa pamoja na kutofuata maadili ya kazi imeelezwa kuwa ni matokeo ya malezi mabaya.
Hayo yalielezwa na Naibu Msaidizi wa Askofu Jimbo katoliki la Moshi,Deodatus Matika katika mahafali ya 24 ya kidato cha nne katika sule ya sekondari ya Ungwasi inayomilikuwa na kanisa katoliki iliyopo Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro.
Alisema kuwa malezi bora yanaanzia tangu utotoni kwa wazazi kuhakikisha kuwa watoto wanafundishwa maadili mema hadi wanapofikia umri wa kuanza shule pia wazazi wanatakiwa kutoa ushirikiano kwa waalimu katika kujenga maadili bora kwa watoto bila kuwaachia jukumu hilo waalimu.
Matiko alisema kuwa maadili yakipungua Nchi itakuwa na jamii isiyofaa,pamoja na kukidhiri kwa vitendo viovu ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya,uhuni ulevi,ambavyo vitachangia kuongezeka kwa umaskini.
“Chanzo cha kuporomoka kwa maadili katika jamii inatokana na wazazi au walezi kusahau wajibu wao kutokana na baaadhi yao kuficha maovu ambayo yamekuwa yakifanywa na vijana bila kuyakemea”Alisema Matiko.
Msaidizi wa Askofu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo aliomba Serikali kuzifikiria shule za binafsi kwa kutoa ruzuku ili kuweza kuboresha zaidi utoaji wa huduma hiyo,pamoja na kuweka mazingira ya shule kuwa mazuri pamoja na kuwalipa wafanyakazi mishahara itakayowafanya kufanya kazi kwa moyo.
Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake Philensia Felichezmoalibainisha kuwepo kwa changamoto mbalimbali ikiwemo tatizo la maji ambalo limekuwa likianza mwezi septemba na novemba hivyo wanafunzi kulazimika kutumia muda mwingi katika kufuatilia maji katika mto Ungwasi uliopo karibu na shule hiyo.
No comments:
Post a Comment