SHIRIKA la utangazaji la Ujerumani (Deutsche Welle) Limeendelea kuimarisha huduma zake nchini Tanzania kwa kuungana na Vodacom Tanzania kwa kurusha kipindi cha ‘Learning by Ear” kwa njia ya simu.
Kuanzia Septemba nane mwaka huu, hadithi fupi maarufu ya redio inayorushwa na DW, inayojulikana kama “Learning by Ear”, itapatikana kwa mahitaji kwa watumiaji wa huduma za simu.
Programu hii inawalenga vijana ambapo inatoa elimu juu ya masuala ya UKIMWI, haki za binadamu, demokrasia, na mazingira ikiambatana na simulizi na makala mchanganyiko za kisisimua na kuburudisha.
Learning by Ear inatolewa katika luga zote zinazotumika katika programu za radio hiyo inayolenga wasikilizaji wa kiafrika. Tayari inarushwa hapa Tanzania kama majawapoza programu za DW-RADIO/Kiswahili.
Deutsche Welle’s kwa Kiswahili ni kati za programu za radio hapa nchini, ambapo inakadiriwa kuwa takiriban silimia 70 ya watanzania wanafahamu Deutsche Welle radio na kila theluthi moja ni msikilizaji wa mara kwa mara wa programu za Kiswahili zinazo rushwa na radio hii.
Mbali na kurusha matangazo yake kwa luga ya Kiswahili, radio hii pia hutoa habari kwa njia ya ujumbe fupi (sms-news) za kila siku kupitia simu za mkononi, tovuti iliyosheheni habari nyingi muhimu (www.dw-world.de/kiswahili), mtandao wa kijamii kama Twitter na Facebook.
Wateja wa Vodacom ambao wamejiunga na huduma ya “Music Radio”, kutoka Vodacom Tanzania, wanaweza wakapata sehemu zote za kipindi cha “Learning by Ear” kwa bei ya kipekee itakayotegemea matumizi kwa sekunde.
Wateja watatakiwa kupiga namba 09011 22 201 kwenye simu zao ili kupata huduma ya ‘music services’ na watatakiwa kusikiliza maelekezo ya namna ya kupata mitiririko mbalimbali ya vipindi cha ‘Learning by Ear ’.
Learning by Ear ilianzishwa kama kipindi cha Deutsche Welle mwaka 2008 kwa Afrika, kwa ushirikiano na Ofisi ya kimataifa ya mambo ya nje ya Ujerumani, na ni moja ya vipindi vilivyofanikiwa sana kwa wasikilizaji vijana.
Kipindi hicho kwa sasa kinazalishwa kwa ushirikiano na marafiki walioko Afrika na kuandikwa na Wahariri wa kiafrika. Zaidi ya vituo vya radio 270 kutoka Nchi mbalimbali za Afrika zinarusha kipindi hicho tangu kianzishwe mwaka 2008, na kukifanya kupata tunzo nyingi ikiwamo ile ya ‘kipindi chenye ubunifu wa juu kwa Radio’ ya mwaka 2009 kutoka Chama cha Kimataifa cha Utangazaji(AIB).
Deutsche Welle ni kituo cha utangazaji cha Ujerumani,ikiwa na vituo kama DW-TV, DW-RADIO na DW-WORLD.DE, zote zikiwa zinazalisha habari, kuangalia tamaduni mbalimbali duniani kote na kuandaa midaalo ya kubadilishana tamaduni.
Vodacom Tanzania Ltd ni kampuni ya mtandao wa simu inayotoa huduma za mawasiliano ya GSM kwa wateja zaidi ya milioni 9 nchi nzima kwa sasa.
Hivi karibuni Vodacom ilizindua huduma ya haraka ya Radio na Tv kwa njia ya simu, kwa kutumia mtandao mpana ilionao nchi nzima na bado kampuni inaendelea na tafiti kwa ajili ya huduma zitakazowanufaisha watanzania zaidi.
No comments:
Post a Comment