Thursday, September 8, 2011

dereva wa boda boda afariki dunia kwa ajali leo

Boda boda yenye nambari za usajili T 592 BAZ ikiwa iko chini mara baada ya kusababisha ajali mbaya sana iliyopelekea kufariki dunia papo hapo kwa dereva wa bodaboda hiyo mara baada ra kugongwa na gari aina ya Land Cruser VX lenye nambari za usajili T 101 BGW leo maeneo ya kijiji cha Mandera nje kidogo ya mji wa Chalinze mkoani Pwani.ajali hiyo imetokea mapema lea asubuhi baada ya bodaboda hiyo kuingia kwenye barabara kubwa bila ya kuwa na tahadhali,ambapo dereva wa gari hilo lililokuwa likitokea Segera kuelekea Dar alijaribu kuikwepa bodaboda hiyo bila mafanikio na hatimae gari hilo likapinduka mara tatu na kuingia kichakani kama inavyoonekana pichani.watu waliokuwepo kwenye gari hilo wametoka salama ila ni dereva wa pikipiki (bodaboda) hiyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja ndie aliefariki dunia.
Gari ikiwa kichakani mara baada ya kupinduka mara tatu kutokana na kujaribu kuikwepa boda boda iliyoingia barabarani ghafla na kupelekea kuigonga na kusababisha kifo cha dereva wa pikipiki hiyo.
Askari wa Usalama Barabarani akiikagua gari hiyo.
Mashuhuda waliokuwepo wakati ajali hiyo inatokea.
Taswira kwa hisani ya Michuzi blog

No comments: