Thursday, September 22, 2011

Kamati ya mambo ya Nje kutoka Bunge la Finland yatembela Bunge

Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama ya Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) akieleza nafasi ya Bunge katika Maswala ya Mambo ya Nje kwa Mwenyekiti wa Kamati ya mambo ya Nje kutoka Bunge la Finland Mhe. Ine Marie Erikson (Mb) mara baada ya kamati hiyo kutoka Finland kutembela Bunge la Tanzania kwa ziara ya kubadilishana uzoefu.
Ujumbe wa kamati ya Mambo ya Nje kutoka Bunge la Finland ukiwa katika kikao cha pamoja na wabunge wa Tanzania kubadilishana uzoefu kuhusu uendeshaji wa shughuli za kamati hususani katika maswala ya uhusiano wa kimataifa. Kamati hiyo kutoka finland ilikutana na Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama ya Bunge na wabunge kutoka kamati nyingine.
Ujumbe wa kamati ya Mambo ya Nje kutoka Bunge la Finland ukiwa katika kikao cha pamoja na wabunge wa Tanzania kubadilishana uzoefu kuhusu uendeshaji wa shughuli za kamati hususani katika maswala ya uhusiano wa kimataifa.
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama ya Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao na Kamati ya mambo ya Nje kutoka Bunge la Finland iliyofanya ziara katika Bunge la Tanzania kwa lengo la Kubadilishana uzoefu
Wajumbe wa kamati ya mambo ya nje kutoka Finland wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama ya Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) pamoja na baadhi ya wabunge wa Bunge letu.
Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge

No comments: