Saturday, April 7, 2012

Fahamu Wasifu wa Marehemu Steven Charles Meshak KanumbaWENGI wamekufa, katika tasnia ya Filamu na maigizo hapa nchini, lakini kifo cha Steven Kanumba "The Great Pioneer" kinasemwa kuwa ni kifo kilicho leta kishindo na mshtuko mkubwa sana miongoni mwa wasanii na wapenzi wa filamu hapa nchini.

Mitandao mingi ya kijamii imetapakaa habari mbalimbali juu ya Kifo cha Msanii wa Magizo na filamu nchini Tanzania, Steven Kanumba.

Steven Charles Kanumba ndio jina lakehalisi akiwa ni mtoto pekee wa kiume katika familia ya Bwana na Bibi, Charles Meshak Kanumba.

Kanumba alizaliwa yeye na dada zake wa wili huku yeye akiwa ni mtoto wa mwisho katika familia hiyo. 

Alizaliwa januari 8, 1984, akiwa ni Msukuma kutoka mkoani Shinyanga alipata elimu yake ya Msingi katika shule ya Msingi Bugoyi mkoani humo.

Alipo maliza elimu yake ya Msingi Kanumba alijiunga na elimu ya Sekondari katika shule ya Mwadui seminari na baade alipofika kidato cha pili kuhamia katika Shule ya Christian a Seminari iliyopo jijini Dar es Salaam.

Alihitimu kidato cha sita katika shule ya Sekondari Jitegemee inayomilikiwa na Jeshi .
Kanumba aliwahi simulia kuwa uigizaji ni kitu ambacho kipo katika damu yake na alikuwa akikipenda na kutamani kuwa mwigizaji tangu akiwa mdogo. Alianza uigizaji akiwa mdogo kwa kufanya maigizo Kanisani.

Mbali na Uigizaji Kanumba pia alipenda sana kuimba na alifanya hivyo akiwa kanisani na shuleni.

Baada ya kuambiwa na watu kuwa anakipaji cha kuigiza ndipo Marehemu Kanumba alipoamua kujiunga na kundi la Kaole ambalo lilikuwa na waigizaji wakongwe ambao hivi sasa baadhi yao wamefariki kama akina mzee Kipara, Pwagu na wengine waliopo kama akina Bui Mwenda, Mashaka na wengine wengi.Kanumba akiwa katika kundi hilo mbali  ya kukutana na wasanii hao wakomngwe ambao alijifunza mengi lakini pia alipata kufundishwa akiwa hapo na walimu kadhaa kutoka chuo cha Sanaa Bagamoyo.

Kanumba baada ya kukaa kwa takribani mwaka mmjoa akijinoa na Kaole sanaa Group alipata mafunzo pia ya uigizaji kutoka Chuo Kikuu cha  Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Dkt Nyoni ambaye alimfunza kwa miezi 3.

Hakika ni kipaji chake cha uigizaji mahiri na kuipenda kazi yake ndivyo viliweza kumjengea jina marehemu Kanumba na hatimaye kuweza kuanza kuteka hisia za watu na mashabiki.

Kanumba alijizolea Sifa nyingi sana ambazo kwa kiasi kikubwa zimemletea mafanikio katika tasnia ya filamu hapa nchini.

Kanumba baada ya mafanikio hayo katika uigizaji alimua kupiga hatua mbele na kuingia katika ulingo wa utengezaji wa filamu hapa nchini.

Katika filamu napo Kanumba amefanya fyema na kutamba vilivyo katika ualimwengu huu wa Filamu za Bongo “ Bongo Movie” na kulishika vilivyo soko hilo la filamu hapa nchini.Kanumba aambaye ametutoka ghafla kwa maana ya bila kuugua na kifo chake kustua wengi hasa katika mapenzi yao makubwa katika filamu zake wataendelea kumkumbuka katika filamu zake kali za kusismua na mafunzo lukuki za Kiswahili.

Miongoni na Big Dady, Because of You, Devel Kingdom, Moses, This is It, More Than Pain, Off Side, Uncle JJ, The Shock na Description filamu iliyopo sokoni hivi sasa ni Kijiji cha Tambua HAKI na hivi karibuni alikuwa njiani kuzindua filamu yake mpya ya Ndoa Yangu.

Ni filamu ambazo hizi ambazo ziliweza kumzungusha Kanumba katika nchi mbalimbali duniani kama Nigeria, Ghana, Amerika na ulaya katika ama kurekodi filamu hizo au kukutana na watu mbalimbali wa tasnia yake na kujifunza mengi.

Zipo Filamu kati ya hizi ambazo ameigiza na waigizaji kadhaa kutoka Nigeria na Ghana.

Kanumba alipata mwaliko wa kushiriki katika tamasha kubnwa la Filamu la Nchini Ghana ambalo linajulikana kamam Festival of Films in Africa (FOFA 2012) lililofanyika katika mji wa Accra Ghana.

Hapa nchini Kanumba atakumbukwa sana na wacheza filamu na wazalishaji kama yeye ambao katika uhai wake aliwahi kufanya nao kazi kama vile Pitchou Mwamba, Ray, Aunt Ezekiel, JB, Wolper, Irine Uwoya, Aunt Ezekiel, Lulu, Jenifer,  Patrick, Sofia, Rich Rich, na wengineo kibao.

Nje yamipaka ya Tanzania kanumba amewahi kuigiza filamu zake hizo na wasanii Nollywood kule  Nigeria na alipata pia kutembelea ngome ya Hollywood, Warner Bros Pictures, Universal Studios na Disney Land.

Kanumba katika vitu ambavyo aliwahi kuvitamka kuwa anavipenda ni watoto nadhani ndio maana hata katika moja ya filamu zake aliigiza na watoto tu Jeniffer na Patriki katika Filamu ya Uncle JJ na hivi karibuni aliongeza mtoto mwingine machachari Sofia.

Pia alipenda kujichanganya na marafiki na kuwa na mitoko kiasi na kupebnda sana kuangalia filamu.

Huyu ndiye Marehemu Steven Charles Kanumba niliyemfahamu. 
Imeandikwa na Father Kidevu (Mroki Mroki) Blog

1 comment:

Rajabu nzowa said...

Jamani kweli hujafa hujaumbika.mwenyezimungu ilazeroho ya marehemu mahali pema peponi.pa poleni familia ya marehemu steven chalse kanumba kwa msiba uliowakumba