Katibu mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Bw. Sethi Kamuhanda (katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) jana jijini Dar es salaam kuhusu matumizi ya nembo ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara na maonesho makubwa ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara yatakayofanywa na Wizara hiyo eneo la Butiama, Musoma kuanzia tarehe 7-14 Oktoba na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kushiriki maonesho hayo na kuitumia nembo hiyo kwenye shughuli mbalimbali zikiwemo za biashara .Kushoto ni Bw. Mulwa Msongo Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu na Bw. Raphael Hokororo (kulia) Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Habari.
Msanii na kiongozi wa B. Band Banana Zolo (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo) pichani kuweka msisitizo wa ushiriki wa wasanii wa kizazi kipya na wale wakongwe katika Tamasha la pamoja la maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara jana jijini Dar es salaam. Wengine ni Said Fella mwakilishi wa kundi la TMK Family (wa pili kutoka kushoto),Mzee King Kii (katikati) na Bw. Waziri Ally.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
No comments:
Post a Comment