Friday, September 9, 2011

WAGOMBEA UDIWANI WA CCM IRINGA WAREJESHA FOMU NDELEMO ZATAWALA MITAANI


Mgombea udiwani wa kata ya Kitanzini kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Jesca Msambatavangu (kulia) akirejesha fomu yake leo kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata hiyo Raphael Magata wengine pichani kutoka kulia ni mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Lediana Mng'ong'o ,katibu wa UWT mkoa wa Iringa Christina Kibiki na katibu wa CCM kata ya Kitanzini Rayson Shayo


WAGOMBEA udiwani wa chama cha mapinduzi (CCM)wauteka mji wa Iringa katika zoezi la urejesha fomu na kupelekea baadhi ya shughuli kusimama katika maeneo ambayo misafara hiyo ilipata kupita.

Wagombea hao Jesca Msambatavangu kata ya Kitanzini Miyomboni na Nicolina Lulandala kata ya Gangilonga walirejesha fomu zao kwa nyakati tofauti katika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi Gangilonga na Kitanzini .


Hata hivyo baadhi ya shughuli za biashara katika maeneo ya uhindini na stendi kuu ya mabasi ya mikoani zilisimama kwa muda kupisha msafara huo wa mgombea wa kata ya Kitanzini Miyomboni Jesca Msambatavangu aliyeanza kurejesha fomu majira ya saa tano asubuhi .

Hali hiyo ndiyo iliyoonekana katika kata ya Gangilonga wakati Lulandala akirejesha fomu katika ofisi ya msimamiazi msaidizi wa uchaguzi kata ya Gangilonga baada ya wananchi wa maeneo ya sabasaba na wilolesi kusitisha shughuli zao kwa muda.

Wakizungumza baada ya kurejesha fomu wagombea hao Msambatavangu na Lulandala walisema kuwa wanaimani kubwa ya kushinda katika kata zao na kuomba wananchi wa kata hiyo kuwaunga mkono kwa kujitokeza kuwapigia kura.

Msambatavangu alisema kuwa imani kubwa ambayo wana CCM waliitoa kake kwa kumpitisha kuwa mgombea wa nafasi hiyo na imani ndioa ambayo anaomba wana CCM na wananchi wote wa kata hiyo kuonyesha siku ya kupiga kura katika kata hiyo.

Huku akieleza kuwatumikia zaidi pindi watakapo mpa nafasi ya kuwa diwani wa kata hiyo.

Huku Lulandala akiwahakikishia makubwa zaidi wakazi wa kata ya Gangilonga iwapo watampa kura na kuwa yupo tayari kufanya vema katika kata hiyo .

Lulandala angombea nafasi hiyo kuziba pengo lililoachwa wazi na aliyekuwa diwani wa kata hiyo marehemu Abubakari Mtamike aliyefariki duni siku ya mbili baada ya kuapishwa kwa diwani wa kata hiyo huku Msambatavangu anagombea nafasi hiyo baada ya kuachwa wazi na marehemu Mariam Nyanginywa aliyefariki hivi karibuni .

No comments: