Friday, September 2, 2011

Matokeo Ya Watahiniwa waliofanya Mtihani Wa Dini Ya Kiislamu Darasa La Saba Yatajwa


(Na Salama Juma)
Maelezo
Mratibu wa mtihani wa dini ya Kiislamu Ustadh Suleyman Dawud ametangaza rasmi matokeo ya watahiniwa waliofanya mtihani wa dini hiyo hapo leo ambao uliofanyika tarehe 10 Agosti, mwaka huu uliohusisha watahiniwa 15,236.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari Maelezo jijini Dar es salaam Mratibu huyo amesema kuwa idadi ya watahiniwa kwa mwaka huu imeongezeka ukilinganisha na miaka iliyopita kwa sababu idadi ya watahiniwa imepanda hadi kufikia asilimia 62.11 ikiwa ni ongezeko la wanafunzi takribani 9,463.
Ustadh Dawud amefafanua kuwa jumla ya watahiniwa 24,699 walifanya mtihani wa kuhitimu Elimu ya Msingi wa dini ya Kiislamu ikiwa ni wanafunzi kutoka shule zipatazo 516 katika mikoa 20 na wilaya 46 ukitofautisha na mwaka 2010 ambapo shule zilikuwa 320 za kote nchini.

Ustadh Dawud ameitaja baadhi ya mikoa iliyoshiriki kuwa ni pamoja na Arusha,Dar Salaam,Dodoma Kagera , Kaskazini Pemba na Tabora.
Amebainsha pia ubora wa ufaulu wa kimkoa nafasi ya kwanza imechukuliwa na Kaskazini Pemba yenye takribani asilimia 76.22 ikifuatiwa na mkoa wa Dodoma wenye takribani asilimia 67.4 ikikamilishwa na mkoa wa Kusini Pemba kwa takribani asilimia 61.55.
Ustadh Dawud amezitaja shule nyingine zilizofanya vizuri kitaifa kuwa ni pamoja na Kamachumu - asilimia 83.38, Jamia - asilimia 80.76, Mwisi mkoani Singida kwa asilimia 78.00, na Wete Islamic ya mkoa wa Kaskazini Pemba kwa asilimia 76.22
Aidha Ustadh Dawud amewataja baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa kuwa ni Abubakari Mstafa Hassan wa shule ya Maji Matitu iliyopo mkoani Dar es salaamkwa aliyepata wastani wa asilimia 96 na kushika nafasi ya kwanza akifuatiwa na Fauza Salehe kutoka ktika shule ya Kamachumu aliyepata asilimia 94 sanjari na Hassan Hamad kutoka katika shule hiyo hiyo.
Ustadh Dawud amewataja watahiniwa 10 waliofanya vizuri katika kila mkoa mikoa hiyo kuwa ni kutoka Arusha, Dodoma,Dar es Salaam, Kagera, Kaskazini Pemba, Singida na Katavi.
Akamalizia kwa kusema kuwa, ufaulu mkubwa wa watahiniwa hao waliohitimu Elimu ya msingi wa elimu ya dini ya kiislamu umechangiwa sana na maandalizi yaliyobora.

No comments: