Saturday, September 3, 2011

CCM Yaibuka 'Kidedea 'Uchaguzi Mwenyekiti Wa Halmashauri Ya Rungwe


CHAMA cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya kimeshinda kwa kishindo nafasi ya mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe kwa kuwabwaga wapinzani katika uchaguzi huo mdogo.Uchaguzi huo ulifanyika ili kuziba pengo liloachwa wazi na aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo aliyeuwawa mwanzoni mwa mwaka huu kwa kupigwa risasi.
Habari kutoka Rungwe zinaripoti kuwa katika uchaguzi huo wajumbe wamemchagua kwa kura 40 aliyekuwa makamu mwenyekitiwa halmashauri hiyo, Meckson Mwakipunga (pichani) huku mgombea wa NCCR Mageuzi,Anyimike Mwakasikilali akiambulia kura 3 tu.

(francisgodwinblog)

No comments: