Wednesday, September 7, 2011

MBUNGE MR. SUGU ALIFYATUKIA JESHI LA POLISI

Na Esther Macha, Mbeya
JESHI la polisi nchini limeonywa kutumia maslahi yao binafsi kwa kuwadhalilisha kwa kuegemea upande mmoja kwa vyama vya siasa kwa kutumia polisi wa ngazi za chini hali inayopelekea kujenga hisia Taifa la kipolisi kataika Tanzania huru.
Kauili hiyo ilitolewa jana na Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi a.k.a MR Sugu pichani (chadema)katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya sido Jijini hapa.
Bw. Mbilinyi alisema kuwa viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakitekeleza majukumu yao kwa mujibu wa katiba ya nchi wala si kuwachochea wananchi kuichukia serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kwamba vitisho hivyo havitawakatisha tamaa kuendelea kuwaelimisha wananchi kudai haki zao.
Akiwahutubia wananchi wa jimbo hilolo huku akiwa ameambatana na Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (Chadema),pamoja na kada machachari wa chama hicho Bw.Fred Mpendazoe alisema kuwa sasa ifikie wakati jeshi la polisi lisitoe vitisho kwa upinzani tu bali hata kwa chama tawala kilichopo madarakani.
Aidha Sugu aliwata wananchi hao kutokubali Propaganda za serikali za kuwatisha viongozi wa upinzani na wabunge wa upinzani kwa kuwaweka ndani mara kwa mara ili waonekane wanavurugu hivyo hawawezi kuwaletea maendeleo.
“ kamwe vitisho hivyo havitawavunja moyo katika harakati za kuwaelimisha na kuwachochea wananchi kuidai serikali yao iwajibike kwao kwa kuwa hilo ni jukumu lao kwa mujibu katiba ya nchi iliyopo”alisema.
Hata hivyo alisisitiza kuwa jeshi polisi likumbuke kuwa hata askari wa Misri walikuwa na magari ya yenye maji ya kuwasha wananyotutishia nayo sasa,lakini wananchi waliposukumwa na nguvu ya mabadiliko hawakujali .
Aidha Sugu alisema katika jimbo lake jeshi la polisi mkoa limekuwa likivunja sheria ya haki za binadamu kwa kuwachanganya mahabusu ,ambapo mahabusu watu wazima huchanganywa na watoto katika vituo vya polisi hali ambayo ni kinyume na sheria na kuwanyima haki zao za
Alitoa ushahidi kuwa wakati alipokamatwa juni mwaka huu kwa kosa la kufanya mikutano bila kibali,alishudia vitendo vichafu vinavyofanywa na askari polisi katika mahabusu ya kituo kikuu cha polisi Mbeya kwa kumpa upendeleo raia mmoja wa kigeni ingawa hakumtaja jina na taifa alilotoka (Mzungu) kwa kumtoa usiku kutoka kwenye chumba cha mahabusu na kwenda kumlaza chumba kingine na kumuwekea godoro jambo ambalo ni kinyume na taratibu.
Kwa upande wake Mchungaji Peter Msigwa(CHADEMA) aliwataka wananchi wa Mbeya kutokubali kurubuniwa na serikali ya CCM kuwa inawaletea maendeleo,badala yake waendelee kuunga mkono upinzani ambao wabunge wake wameleta mabadiliko makubwa ndani ya bunge la muungano.
Aidha,Mchungaji Msigwa alisema ndani ya CCM hakuna mwenye uthubutu wa kumnyooshea kidole mwenzake juu ya tuhuma za ufisadi kwa kuwa kila mmoja wapo wa viongozi wa juu alihusika kufanya ufisadi kwa taifa.

No comments: