Sunday, September 11, 2011

NBC yasaidia wahanga wa ajali ya meli zanzibar

Waziri wa Afya wa Zanzibar, Juma Haji Duni (katikati) akizungumza baada ya kupokea msaada wa vyakula, dawa, maji na misaada mingine ya kibinadamu iliyotolewa na Benki ya NBC kwa ajili ya wahanga wa ajali
ya Meli ya MV Spice Islander iliyotokea usiku wa Septemba 10 visiwani humo. Katikati ni Mshauri wa Mambo ya Habari wa NBC, Redemptus Masanja na nyuma ya Masanja ni Ofisa Uhusiano wa benki hiyo, Eddie Mhina. Hafla ilifanyika Zanzibar juzi
Mshauri wa Mambo ya Habari wa Benki ya NBC, Redemptus Masanja (kushoto) akikabidhi sehemu ya misaada iliyotolewa na NBC kwa ajili ya wahanga wa ajali ya Meli ya MV Spice Islander kwa Waziri wa Afya wa Zanzibar Juma Haji Duni Mjini Zanzibar juzi. Kulia ni Meneja wa Tawi la NBC Zanzibar, Rajab Maalim
Meneja wa Tawi la Benki ya NBC Zanzibar, Rajab Maalim (kulia) akizungumza katika hafla ambayo NBC ilikabidhi msaada wa vyakula, dawa, maji na misaada mingine ya kibinadamu iliyotolewa na benki hiyo
kwa ajili ya wahanga wa ajali ya Meli ya MV Spice Islander iliyotokea usiku wa Septemba 10 visiwani humo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika visiwani humo mwishoni mwa wiki. Katikati ni Waziri wa Afya wa Zanzibar, Juma Haji Duni na wa pili kushoto ni Mshauri wa Mambo ya Habari wa NBC, Redemptus Masanja.
Ofisa Uhusiano wa NBC Tanzania, Eddie Mhina (wa pili kushoto) akisaidiana na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo na wakazi wa Zanzibar kushusha baadhi ya vitu vilivyotolewa msaada na benki hiyo kwa ajili ya wahanga wa ajali ya Meli ya MV Spice Islander iliyotokea usiku wa Septemba 10 visiwani humo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika Visiwani Zanzibar juzi.
Waziri wa Afya wa Zanzibar, Juma Haji Duni (kushoto) akipokea msaada wa vyakula, dawa, maji na misaada mingine ya kibinadamu iliyotolewa na Benki ya NBC kutoka kwa Meneja wa Tawi la benki hiyoVisiwani Zanzibar, Rajab Maalim kwa ajili ya wahanga wa ajali ya Meli ya MV Spice Islander iliyotokea usiku wa Septemba 10 visiwani humo.. Hafla ilifanyika Zanzibar juzi.

No comments: