Tuesday, September 6, 2011

Rais Kikwete Aizawadia NSSF kwa Mchango katika ujenzi

Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika ufunguzi wa Mkutano wa siku tatu unaojumuisha wahandisi, Wabunifu majengo, Wakadiriaji na Makondrasi uliofanyika leo Mlimani City,jijini Dar es Salaam.
Rais Dr. Jakaya Kikwete (wapili kushoto) akimkabidhi Cheti,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dr. Ramadhani Dau (wa pili kulia) kwa kutambua mchango mkubwa wa Mfuko huo katika sekta ya ujenzi hapa nchini.Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Dr. John Magufuli.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dr. Ramadhani Dau
(kulia) akiwa ni mwenye furaha mara baada ya kukabidhiwa Cheti na Rais Kikwete ikiwa ni kutambua mchango mkubwa wa Mfuko huo katika sekta ya ujenzi hapa nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dr. Ramadhani Dau
pamoja na wadau wengine wakifatilia mkutano huo.

Picha ya Pamoja.

Na Alfred Ngotezi

Rais Jakaya Kikwete leo amemkabidhi Cheti Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dr. Ramadhani Dau kwa kutambua mchango mkubwa wa Mfuko huo katika sekta ya ujenzi hapa nchini.

Rais Kikwete ambaye alikuwa mgeni kwenye ufunguzi wa Mkutano wa siku tatu uliojumlisha wahandisi, Wabunifu majengo, Wakadiriaji na Makondrasi alitoa zawadi hiyo kwa niaba ya Bodi ya Wakondrasi.

Mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya watu, kutoka nje na ndani, ulianza tarehe 5 na utakwisha tarehe 7 Septemba mwaka huu. Baadhi ya wajumbe walitoka Afrika Kusini, Zambia, Kenya na Malawi.

Akiongea kwenye hafla hiyo fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City mjini Dar es Salaam, Rais aliwapongeza Wahandisi, Wabunifu Majengo,Wakadiriaji na Makondrasi walioandaa mkutano huo na kuwataka wajiunge pamoja ili waweze kupata uwezo mkubwa wa kufanya kazi.

Katika siku za karibuni NSSF imekuwa na miradi mikubwa ya ujenzi. Baadhi ya miradi hiyo ni ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, nyumba za Polisi Dar es Salaam na Zanzibar na nyumba za Jeshi huko Monduli Arusha. Hivi karibuni NSSF itaanza kujenga Daraja la Kigamboni.

No comments: