--
Akizungumzia habari iliyochapishwa na gazeti hilo,Mheshiniwa Ndasa alisema kuwa gazeti la Mwanahalisi limechapisha habari za kizushi na za uongo zenye lengo la kufitinisha Bunge na Rais.Aliongeza kusema kuwa wakati Jairo anarudishwa kazini na Katibu Mkuu, Luhanjo, Bungeni mjini Dododma hapakuwa na hatua yoyote ya wabunge kupanga kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais kufuatia kuruhusiwa kwa Jairo kuendelea na kazi.
Akifafanua kuhusu uamuzi wao wa kutolea ufafanuzi na kukanusa habari hiyo, Ndasa alisema wao kama wabunge wa CCM, hawatopenda kuona kiongozi wa nchi anazushiwa habari zisizo na ukweli wowote.
Akijibu swali kwa nini wao kama wabunge wajitokeze kukanusha taarifa hiyo ikiwa Ikulu ina kurugenzi ya Mawasiliano, Bunge linaongozwa na Spika, Pia yupo Waziri mkuu, ambaye ni kiongozi wa shughuli za serikali bungeni ambao kimsingi moja kati ya mamlaka hizo ndizo zilizotakiwa kufafanua au kukanusha habari hiyo, Ndasa alisema, wao hawajatumwa na Ikulu wala mamalaka yoyote bali wametumwa na dhamira yao kama Watanzania
No comments:
Post a Comment