Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa tuzo na Waziri Mkuu wa Antigua and Barbuda Mh. Winston Baldwin Spencer kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya afya, teknolojia na maendeleo kwenye hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na taasisi ya South-South katika hoteli ya Waldorf Astoria jijini New York Jumatatu usiku.(Picha kwa hisani ya Ikulu)
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa shukrani kwa kupewa tuzo hiyo. Marais Paul Kagame wa Rwanda, Abdoulaye Wade wa senegal na Mwai kibaki wa Kenya, pia walipokea tuzo kwa michango yao katika maendeleo ya nchi zao
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Dkt Marion Bergam, Mkurugenzi wa miradi ya Health Care Projects ya Miracle Corners of the World katika mkutano wa kwanza wa kuhimiza hatua zichukukuliwe dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza, hususan ya kinywa. Serikali ya Tanzania ndiyo iliyodhamini mkutano huo uliofanyika Chuo Kikuu cha New York kitivo cha meno
Mwanamuziki maarufu wa Afrika Kusini ambaye ni Balozi wa heshima wa Roll Back Malaria Yvonne Chakachaka akiendesha shughuli hiyo kama MC
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Dkt Asha Rose migiro kwenye hafla hiyo ya Roll Malaria
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati wa hafla ya kupongeza mafanikio ya juhudi za kupambana na ugonjwa wa malaria ya Roll Back Malaria katika hoteli ya Intercontinental jijini New York

No comments:
Post a Comment