Saturday, September 17, 2011

Rais wa Zanzibar Dr Shein Atoa Pole kwa wananchi wa Pemba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi waliofiliwa na ndugu zao katika Ajali ya meli ya Mv Spice Islander,katika mkondo wa Nugwi,mazungumzo hayo yalifanyika jana katika ukumbi wa Umoja ni Nguvu Mkoani Pemba.
Wananchi wa wilaya ya Mkoani Pemba,waliofiliwa na jamaa zao katika ajali ya meli ya Mv Spice Islander,iliyotokea wiki iliyopita katika mkondo wa Nungwi,kasakazini Unguja,wakiitikia dua iliyoombwa na sheikh Hamadi Juma,baada ya mazungumzo na Rais wa Zanzibar alipofika kuwapa pole katika ukumbi wa umoja ni nguvu Mkoani Pemba.
wanananchi wa Wilaya ya Chake chake Pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,alipokuwa na mazungumzo na wananchi hao,katika uwanja wa Gombani,alipowapapole ya kufiliwa na jamaa zao,kutokana na jamaa zao kwa ajali ya kuzama meli ya Mv Spice Islander,huko katika mkondo wa nungwi hivinkaribuni.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Mama Mwanamwema Shein,akiwapa pole wananchi wa wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba,waliofiliwa na jamaa zao katika tukiokubwa la kuzama kwa Meli ya Mv Spice Islander,katika mkondo wa Nungwi,huko uwanja wa Gombani jana,katika ziara maalum ya kuwapapole wafiwa kisiwani Pemba.
Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Jabu Khamis Mbwana akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein alipofika kutowa mkono wa pole kwa Wananchi waliofiwa na jamaazao katika ukumbi wa Umoja Mkoani.

No comments: