Saturday, September 10, 2011

RISASI 2200 ZA BUNDUKI ZA KIVITA ZAKAMATWA PAMOJA BAISKERI 5

Baiskeri zirizotumika kusafirishia risasi 2200 kushoto ni RCO Joseph Konyo katikati ni RPC Frasser Kashai ariefuata OC CID Moha
ACP Frasser Kashai akiwa na risasi zilizokamatwa
SSP Joseph Konyo, RCO wa Kigoma, akiwa na risasi hizo

Na Pardon Mbwate wa Jeshi la P olisi Kigoma

Jeshi la polisi mkoa wa kigoma limeendelea kufanya misako endelevu dhidi ya makosa mbalimbali ya jinai yakiwemo unyang’anyi wa kutumia silaha, wahamiaji haramu, madawa ya kulevya na makosa ya usalama barabarani. aidha mbinu mbalimbali zimetumika katika kuleta mafanikio ikiwemo doria, kufanya misako mbalimbali na vizuizi vya barabarani. mafanikio yaliyopatikana ni kama ifuatavyo :-

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma ACP Fraisser Kashai, amesema kuwa jeshi la polisi limefanikiwa kukamata Risasi 2200 mnamo tarehe 07/09/2011 majira ya saa 01:00hrs huko uvinza katika wilaya na mkoa wa kigoma. askari polisi wakiwa kazini katika kizuizi cha barabarani (beria) waliwasimamisha watu watano waliokuwa na baiskeli kila mmoja kwa nia ya kuwapekua baada ya kuwatilia mashaka.

Kamanda Kashai amesema kuwa baada ya kuwatilia muda waliokuwa wakisafiri kwa baiskeli ghafla watu hao baada ya kugundua kuwa walikuwa wamesimamishwa na askari walitupa baiskeli zao na kukimbia huku wakizitelekeza baiskeli zao. vifurushi vilivyokuwa katika baiskeli hizo vilipekuliwa na zilipatikana risasi 2200 za bunduki za kivita aina ya S.M.G. / S.A.R
Aidha Kamanda amesema jumla ya tshs 740,000/= zilikusanywa kama faini za makosa mbalimbali ya usalama barabarani yaliyokamatwa katika operesheni maalumu iliyofanyika kati ya tarehe 08/09/2011 na 09/09/2011
Hata hivyo Kamanda Kashai amesema kuwaJeshi Jeshi la polisi linatoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano katika kufanikisha vita ya kupambana na uhalifu na wahalifu

Sanjari na hilo madereva na wamiliki wa vyombo vya usafiri wanatakiwa kufuata sheria na kuhakikisha magari yao yako katika viwango vya kubeba abiria kwa mujibu wa sheria na kwa mara nyingine ninawaimiza madereva wote ambao reseni zao zimekwisha muda wake kwenda kwenye mamlaka husika na kupata leseni hizo.

No comments: