Sunday, September 11, 2011

TUKIO JIPYA : NI SIKO YA MAJONZI ZAIDI ZANZIBAR

Mtalii toka Ufaransa akisaidia katika kuhudumia walionusurika katika ajali ya meli ya LCT Spice Islanders. Hadi sasa maiti 192 wamepatikana ambapo 17 kati yao wamezikwa na serikali kwa kuwa miili yao imeharibika kiasi cha kutoweza kutambuliwa. Siku tatu za maombolezo zinaanza leo kisiwani Zanzibar ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti na sherehe na starehe zote zimesimamishwa
Watalii wakitoa msaada kwa walionusurika
Shughuli ya uokoaji ikiendelea
Viongozi wakuu wote wakiwa msibani
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakimjulia hali mmoja kati ya majeruhi wa ajali ya Meli iliyotokea eneo la Nungwi, Mussa Hemed, mkazi wa Wete Pemba, aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK, BILAL AKIWA NA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF WAKIMFARIJI MMOJA KATI WA WAHANGA WA MV.SPICE ND MUSSA HEMED ANAETOKEA MJI WA WETE ALIYELAZWA KATIKA HOSPITALI KUU YA MMNAZI MMOJA,
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI ALIPOMTEMBELEA MTOTO SAID JERAD MMOJA WA MAJERUHI WALIOLAZWA KATIKA HOSPITALI KUU YA MNAZI MMOJA, ZAIDI YA 600 WALIOKOLEWA WAKIWA HAI KUFUATIA KUZAMA KWA MELI YA MV. SPICE
NI KIKAO ALICHO KITAYARISHA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR MHE BALOZI SEIF ALI IDDI KWA VIONGOZI WA SERIKALI WALIOKUWEPO KISIWANI PEMBA CHENYE LENGO LA KUWEKA MIKAKATI YA KUKABILIANA NA UPOKEAJI WA WAHANGA WA AJALI YA MELI YA MV SPICE ISLANDERS, KATIKA HICHO WAMEKUBALIANA KUWEKA VITUO VYA DHARULA KATIKA MAENEO YA MKOANI,CHAKE NA WETE ILI KUPOKEA WATU WALIOPATWA NA MAAFA HAYO KWA KUWAPATIA HUDUMA.

Baadhi ya abiria 525 waliookolewa kutoka katika Meli iliozama huko katika mkondo wa Nungwi Zanzibar wakiwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja mjini Zanzibar
Watoto waliookolewa kutoka ktika Meli iliozama ya Spici huko katika mkondo wa Nungwi zanzibar wakiwa katika Hospitali ya mnazi mmoja kabla ya kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Umati wa watu wakiwa katika Hospitali ya mnazi mmoja kupata taarifa za watu wao kuhusiana na kuzama kwa meli ya Spice Islanders huko katika mkondo wa Nungwi
Vikosi vya Ulinzi na Usalama ni miongoni mwa Taasisi zilizokuwa mstari wa mbele katika harakati za uokoaji na usafirishaji wa maiti zilizopatikana kutoka katika meli iliozama ya spici iliokuwa ikielekea Pemba, kama wanavyoonekana katika picha.
Mmoja kati ya waokozi akiwa katika hali ya majonzi baada ya kuchukuwammoja kati ya maiti zilizoletwa bandarini zanzibar na chombo cha bawe kutoka katika meli iliozama huko katika mkondo wa Nungwi.

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akibadilishana mawazo na Naibu kadhi wa Zanzibar kutokana na msiba mkubwa uliotokea zanzibar jana.
Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akizungumza na Madaktari huko katika viwanja vya maisara mjini Zanzibar kuhusiana na Msiba mkubwa ulolikumba taifa letu la kuzama kwa meli ya Spici huko katika mkondo wa Nungwi kaskazini unguja.

Madaktari,Wauguzi na watu mbalimbali wakipokea maiti ya kwanza iliofikishwa huko katika viwanja vya Maisara kutoka katika meli ya spici iliozama hapo jana huko katika mkondo wa Nungwi. PICHA ZOTE NA HAMAD HIJA-MAELEZO ZANZIBAR



Na Hamad Hija Maelezo zanzibar

MAMIA ya wananchi wakiwemo viongozi wakuu walimiminika katika viwanja vya Maisara na Hospital ya Mnazi mmoja pamoja na bandari kuu ya zanzibar ili kwenda kuona na watambuwa watoto wao wazee wao ambao walikuwepo katika meli iliyopata ajali huko Nungwi ikielekea kisiwani Pemba hapo jana

Waliomiminika katika sehemu hizo kutoka sehemu mbali mbali za Unguja kunafuatia habari zilizoanza kutangazwa jana katika vyombo mbali mbali vya habari kwamba chombo cha Spice kimezama na ni kwamba kilikuwa kimechukuwa abiria kikielekea Pemba

Kwa mujibu wa habari zilizokuwa zikisimuliwa na baadhi ya wananchi waliofika hapo maisara wamesema kuwa suala kubwa lililochangia kutokea ajali hiyo ni kuwa vyombo vimechoka sana na wengine wamesema kuwa kujaa sana kwa chombo hicho hapo jana pia ni sababu ambazo zilichangia tukio hilo

Katika Viwaja vya Maisara umati wa watu ulikuwa umejaa kupita kiasi halikadhalika hata Hospital ya Mnazi mmoja umati ulikuwa umejaa vikle vile lengo kubwa la kuwepo hapo ni kuona na kuwatambua vijana wao ambao wameruhiwa na ambao wanapata matibabu

Halikadhalika umati mkubwa ulikuwa umejazana sana katika bandari mkuu ya Zanzibar ambapo maiti na majeruhi wa ajali hiyo walikuwa wakifikia hapo kutoka sehemu ya tokeo

Kufuatia ajali hii hiiitakuwa mara ya pili katika pindi cha nyuma meli ya MV Fathi ilizama ambapo watu kadhaa wafariki dunia na baadhi ya mizigo ilpotea kutokana na ajali hiyo iliyotokea hapo nyuma

Kufuatia tokeo hilo wananchi wa zanzibar leo walikuwa wamejikusanya vikundi kila sehemu kuzungumzia tukio hili ambalo limetoke hapo jana likiwa limeacha majonzi makubwa kutokana na msiba huo uliotokea hapa zanzibar







No comments: