Thursday, September 1, 2011

UVCCM MKOANI MBEYA YAKOSA IMANI NA KATIBU WA CCM.

Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Bi. VERENA SHUMBUSHO.
Jumuiya ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Mbeya Vijijini imekosa imani na Katibu wa chama hicho Nicolaus Kasendamila na kuamua kumtimua.

Uamuzi huo umetolewa na Baraza kuu la vijana hao lililokuwa limeketi katika ukumbi wa mikutano wa Lehner uliopo mjini Mbalizi wilayani humo Agosti 30 mwaka huu na kumwamuru katibu wa vijana na Mwenyekiti kuandika barua ya kumwondoa wilayani humo haraka iwezekenavyo.

Taarifa kutoka ndani ya Baraza hilo zimeueleza mtandao wa www.kalulunga.blogspot.com kuwa hoja ya kutomtaka katibu huyo ilitolewa na mmoja wa wajumbe wa Baraza hilo baada ya kusomwa mrejesho wa uchaguzi mkuu uliopita 2010 ambapo katibu huyo alionekana kuhusika kwa madeni ya jumuiya hiyo na kuwakosesha imani vijana mbele ya jamii.

Chanzo hicho kilisema kuwa Katibu huyo ambaye alikuwa ni mmoja wa wajumbe alijitetea kuwa atalipa madeni hayo na kwamba adhabu hiyo iondolewe dhidi yake jambo ambalo halikukubaliwa na wajumbe huku Mwenyekiti wa UVCCM Samwel Ntenga akifunga agenda hiyo na kuendelea na agenda nyingine.

Taarifa za uchunguzi kutoka ndani ya CCM wilayani humo zimebaini kuwa licha ya Jumuiya hiyo kukitaka chama kumwondoa katiwa huyo, pia Jumuiya ya Wazazi kupitia baraza lake kuu limetoia maazimio hayo ya kukitaka chama hicho kumfukuza kazi Katibu huyo kwa madai kuwa anakiharibu chama hivho wilayani humo.

Mbali na hayo yote, Jumuiya ya Vijana hao imeunga mkono dhana ya kujivua gamba iliyoasisiwa na kamati kuu ya CCM na Sekretarieti yake huku wakionya kuwa dhana hiyo isitumike katika malengo binafsi ya siasa na hisia chafu kwa wengine wanaoonekeana kikwazo kwa waliokabidhiwa dhamana kuieneza dhana hiyo.

Katibu wa UVCCM wilayani humo Frank Kibiki na Mwenyekiti wake Samwel Ntenga walipohojiwa kw njia ya simu na mtandao huu wa www.kalulunga.blogspot.com walithibitisha kuwepo kwa suala hilo lakini walisema kwa sasa suala linalosubiliwa ni wao kuandika yale waliyoagizwa na Baraza kisha kuyapeleka kunakohusika.

No comments: