Monday, September 5, 2011

VODACOM MISS TANZANIA KUONDOKA NA GARI AINA YA JEEP MPYA YENYE THAMANI YA SHILINGI M.72

Meneja
Masoko wa CFAO Motors Alfred Minja kulia na Mkuu wa Udhamini na Masoko
Vodacoma Tanzania George Rwehumbiza wakifunua gari aina ya JEEP ambalo
limetolewa kama zawadi ya Vodacom Miss Tanzania 2011 lenye thamani ya
shilingi milioni 72 za kitanzania gari hilo limetengenezwa nchini
Marekani.


Hafla ya kuonyesha gari hilo la zawadi imefanyika asubuhi hii katika
duka la kampuni ya CFAO Motors lililopo Barabara ya Nyerere jijini Dar
es salaam, kulia anayeshuhudia tukio hilo ni mkurugenzi wa kamati ya
Miss Tanzania Hashim Lundenga.



Meneja
Masoko wa CFAO Motors Alfred Minja katikati na Mkuu wa Udhamini na
Masoko Vodacoma Tanzania George Rwehumbiza wakikabidhi funguo za gari
lililotolewa na kampuni hiyo kama zawadi ya Vodacom Miss Tanzania kwa
Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga



Warembo
watakaoshindania taji la Vodacom Miss Tanzania wakiwa wamelizunguka
gari ambalo lilmetolewa kama zwadi ya mshindi atakayeibuka siku hiyo.



Warembo
wa Vodacom Miss Tanzania wakifurahia zawadi yao gari aina ya Jeep
iliyotolewa na wadhamini wa shindano hilo CFAO Motors na Vodacom
Tanzania.Kwa Hisani Ya Full Shangwe Blogu

No comments: