Na Esther Macha, Mbeya
SHIRIKA la watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Tunduma(SHIWAUTU) wameiomba serikali na vyombo vya kusimamia sheria kuanza kutekeleza sheria ya Ukimwi ya mwaka 2008 inayoelekeza kwamba maambukizi ya kukusudia ni kosa la Jinai.
Mwenyekiti wa shirika la watu wanaoishi kwa uhakika lenye makao makuu yake Mjini Tunduma Bw.Musa Ndoloma alisema idadi kubwa ya watu hususani wanaotumia dawa za kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi-ARV, wamejiingiza tena katika vitendo vya kuambukiza virusi kwa kukusudia,
Alisema kuwa matokeo yake kumekuwepo na ongezeka kwa kiwango cha maambukizi nchini na kuwa ,dawa hizo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kurejesha afya,kurejea kwa afya zao wamejiunga kushiriki vitendo hatarishi vya Ugonjwa wa Ukimwi kwa kushirikiana na watu wengine ambao wanaishi bila ugonjwa huo.
Alisema kuwa ni sita sasa tangu serikali ianze kutoa dawa za kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi kwa waathirika, dawa inayotolewa bila malipo,inadaiwa na wengi kuwa imewasaidia.
Hata hivyo wakizungumza na gazeti hili baadhi ya watu waliojitangaza wazi kuishi na virusi vya Ukimwi ambao ni wanachama Aai wa SHIWAUTU pamoja na mambo mengine wameisifu serikali kwa kuwalipia gharama za dawa hiyo kwa wahisani na kwamba imekuwa ni msaada mkubwa kwao,familia na taifa kwa ujumla.
Walisema kuwa sheria ya Ukimwi ikitumika ipasavyo itakuwa ni msaada kwa kizazi cha sasa hususani vijana ambao wanajiingiza kwenye vitendo vya ngono kutokana na umaskini,lakini wanarubuniwa na wenye pesa,matokeo yake ni kufifisha ndoto zao walizojiwekea.
Aidha Mwenyekiti huyo alisema kuwa kuna idadi kubwa ya wenye pesa ambao wamekuwa wakitumia pesa zao kuwarubuni vijana hali ambayoo sheria hiyo ingetumika ipasavyo ingekuwa chanzo cha kupunguza maambukizi mapya ya virus vya Ukimwi
No comments:
Post a Comment