Na Esther Macha, TGNP Dar
WITO umetolewa kwa jamii kuheshimu kikamilifu haki za binadamu kwa kutowabagua wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzio kwani wengi wao wamekuwa wakidhalauliwa na kutukanwa hivyo kusababisha wasishiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa.
Imeelezwa kuwa jamii ya wanaume hao imekuwa ikidhalauliwa na kuona kama jambo hilo ni kitu cha ajabu huku jamii ikisahau kuwa kila bidanamu anastahili kuheshimiwa na kuthaniwa.
Akizungumza wakati wa Tamasha la Jinsia la 10 Mkurugenzi wa Mkuu Taasisi ya wanawake na vijana kutoka Nairobi Bi. Saida Ally ambalo lilijadili mada ya Udada uwezo, usawa na uadilifu kwa wanaharakati wa kutetea haki za wanawake Tanzania katika Viwanja vya TGNP vilivyopo Mabibo.
Bi. Ally alisema kuwa hata wanawake wapo ambao wanakuwa na mahuasiano ya wao kwa wao na hivyo hivyo wanaume nao wanafanya mapenzi na wanaume wenzio si kwamba wamependa kuwa hivyo bali ni maumbele ambayo wamezaliwa nayo hivyo hawakiwi kunyanyapaliwa na jamii bali wanatakiwa kuwaona kama watu wengine.
“Hawa nao ni ndugu zetu wanahitaji kupata haki kwani kuna mwingine akijulikana anafanya tendo hilo familia humtenga au kumfukuza kwa kuona tendo hilo halifai lakini sasa unakuta mtu wa mjini akimwona mtu wa namna hiyo anashangaa kupita kupita , mtu wa kijijini ndiyo anatakiwa ashangae hivyo ndo maana unakuta watu hawa wamekuwa wakikaa kwa kificho kutokana na jamii kuwashangaa”alisema.
Akichangia mada ya Udada ya Usawa, uwezo na Uadilifu Mwanaharakati ambaye anafanya mapenzi na wanaume wenzake Bw. Abduli Zungu alisema kuwa baada ya kugundulika kuwa anajihusisha na mapenzi ya jinsia moja Baba yake mzazi alimfukuza nyumbani lakini mamaake mzazi alikaa na kumuelewesha mumwe kuwa mwanae pamoja na matendo anayofanya mwanae bado ana haki ya kuishi nyumbani na kuthaminiwa kama binadamu .
“Huu mfumo umekuwa ukitukandamiza sisi wanaume ambao wanapenda kutuita mashoga kuwa hatustahili kufanya kitendo hicho ili hali ni maumbele ambayo tumezaliwa nayo hatuna namna ndo maana tumefika hapa nasi kutetea haki yetu ya kimsingi na mimi binafsi nawapenda san asana wanawake wenzangu mliopo hapa sisi tuna nguvu kwani tunatakiwa kuonyesha upendo kwa waume zetu sisi ni wajasiri wanawaume wanatakiwa kutunyenyekea “alisema Bw. Zungu.
Hata hivyo mwanaharakati huyo alisema wapo katika tamasha hilo kwa ajiri ya kutetea haki yao kwani hata sisi ni moja ya washiriki wa Tamasha hili hivyo lazima kushiriki kikamilifu ili tutoe mawazo wetu na jamii ipate kuelewa.
No comments:
Post a Comment