Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania,Sabasaba Moshingi (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 4 kwa Mbunge wa jimbo la Bukene mkoani Tabora,Mh. Selemani Zedi ikiwa ni msaada uliotolewa na benki hiyo kwa ajili ya kununulia madawati yatakayotumiwa na wanafunzi wa shule za msingi za jimbo hilo.makabidhiano hayo yamefanyika asubuhi hii katika ofisi ya makao makuu ya Benki hiyo,mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania,Sabasaba Moshingi akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi msaada huo kwa Mbunge wa Jimbo la Bukene.
Mbunge wa jimbo la Bukene mkoani Tabora,Mh. Selemani Zedi akitoa shukrani zake kwa uongozi wa Benki ya Posta Tanzania mara baada ya kupokea msaada wa sh. milioni 4 kwa ajili ya kununulia madawati yatakayo tumiwa na shule za msingi za jimboni kwake.
No comments:
Post a Comment