Tuesday, October 25, 2011

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dk Ali Shein Ala Kiapo Ikulu Jijini Dar es Salaam Cha Kuwa Mjumbe na Kushiriki Vikao Vya Baraza la Mawaziri

Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande (kushoto), akimwapisha Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kuwa Mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Tanzania, Ikulu, Dar es Salaam leo(jana)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akipokea hati ya kiapo kutoka kwa jaji Mkuu wa Tanzania Othman Chande muda mfupi baada ya kula kiapo cha kuwa mjumbe na kushiriki katika vikao vya baraza la mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kwa Mujibu wa Katiba ya Jamhuri wa Tanzania Kifungu Namba 54 ibara ya kwanza ambao inawataja wajumbe wa Baraza la Mawaziri Kuwa ni Makamu,Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na Mawaziri Wote.
Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Rais Jakaya Kikwete(Kushoto)akimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri Dk Ali Shein Muda mfupi baada ya kula kiapo cha kuwa Mjumbe na kushiriki katika vikao vya Baraza la Mawaziri Vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Mujibu wa Kifungu Namba 54 ibara ya kwanza ambao inawataja wajumbe wa Baraza la Mawaziri Kuwa ni Makamu,Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na Mawaziri Wote.Picha na Ramadhani Othman Ikulu-Zanzibar



No comments: