Wednesday, October 5, 2011

DEREVA WA LORI LILILOUA 14 MBEYA ASOMEWA MASHTAKA 14 AKIWA KITANDANI

:

Dereva wa gari namba T582 AJF aina ya Fuso lililopata ajali septemba 24 mwaka huu na kuua watu 14 na majeruhi 43 (aliyelala )akisomewa mashitaka 44 na Wakili wa Serikali Bw.Griffin mwakapeje, hayupo pichani (Picha na habari na Esther Macha).



Na Francis Godwin

DEREVA aliyesababisha vifo vya watu 14 katika ajali iliyotokea eneo la Msangamwelu Wilayani Chunya Bw. Moses Kapus (55)amesomewa mashitaka 44 akiwa chini ya ulinzi katika hospitali ya Rufaa Mbeya .

Ajali hiyo ilitokea septemba 24 mwaka huu majira ya saa 1 .00 usiku baada ya roli aina ya fuso lililokuwa likitokea mnadani eneo la Mbuyuni wilayani Chunya kushindwa kupanda mlima na kuanguka.

Akimsomea mashtaka hayo mbele hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya hakimu mkazi wa Wilaya Bw. Michael Mteite Wakili wa Serikali Bw.Griffin Mwakapeje alidai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na makosa 44.

Bw. Mwakapeje alidai kuwa mshtakiwa Kapus akiwa kama dereva alisababisha ajali kwa uzembe kutokana na kuendesha kwa kasi na kusababisha vifo vya watu 14.

Wakili huyo alidai kuwa dereva huyo akiwa na gari aina ya fuso zenye namba T582 AJF aliendesha gari hiyo kwa mwendo wa kasi na kusababisha majeruhi 43 ambao mpaka sasa hali zao hazijaweza kuwa nzuri na kwamba mshtakiwa huyo alitumia gari hilo kinyume na aliyopewa .

Kwa upande wake Hakimu wa Mahakama hiyo Bw.Mteite alisema mahakama imepokea makosa yote alisomewa mshitakiwa 44.

Hata hivyo mshitakiwa aliomba mahakama impe dhamana kutokana na hali yake kuwa mbaya kiafya, ambapo hata hivyo wakili wa serikali alimwomba Hakimu wa mahakama kuwa masharti ya dhamana yaangaliwe kwanza nay awe magumu kutokana na hali za majeruhi kuwa mbaya.Aidha Hakimu huyo alimtaka mshitakiwa kuwa na fedha taslimu sh. Mil.5 na wadhamini wawili wenye nyumba ili aweze kupata dhamana.

Hata hivyo Wakili wa serikali alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kuwa tarehe ya shauri hilo itakuwa Octobar mwaka huu.

No comments: