Monday, October 10, 2011

Dr Bilal Kuzindua Kanuni Za Sheria Ya Filamu Na Michezo Ya Maigizo

Na Ismael Ngayonga, MAELEZO
MAKAMU wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilali anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi kanuni mpya za sheria ya filamu na michezo ya kuigiza ya mwaka 2011.
Akizungumza katika maonyesho ya sherehe za maonyesho ya miaka 50 uhuru wa Tanzania bara kwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini, Joyce Fissoo alisema uzinduzi huo unatarajia kufanyika tarehe 13 oktoba mwaka huu mkoani Mara.
Alisema sheria namba 4 ya bodi ya filamu ya mwaka 1976 haikuwa na kanuni za utekelezaji, hivyo ili tasnia hiyo iweze kuleta tija iliyokusudiwa Serikali imeamua kutunga kanuni mpya.
Fissoo alisema wakati wa kipindi cha utawala wa ukoloni wa waingereza nchini, filamu nyingi zilizoonyeshwa zilikuwa zikisifu utamaduni wa kizungu na hazikuwa katika mfumo wa kibiashara.
Kwa mujibu wa Fissoo alisema mara baada ya uhuru kuliwepo na filamu maalum na maudhui yake yalikuwa ni kuelimisha wananchi na kuwahamasisha kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo kilimo.
Aidha Fissoo alisema mwaka 2000 tansia ya filamu nchini ilkuwa na kushika kasi kwa watengezaji wa filamu wa ndani kuanza kutengeneza filamu zao wenyewe, hatua iliyoibua changamoto mbalimbali katika jamii
“Kutokana na kukua kwa tasnia ya filamu nchini, kumetokea madhara makubwa ya mmomonyoko wa maadili katika jamii ambapo kwa kiasi kikubwa kumetokana na kukua kwa utandawazi na waigizaji na watumiaji wetu walkishindwa kijua ni mapokea gani wayachukue” alisema Fisso
Akifafanua zaidi Fissoo alisema kutokana na hali hiyo, Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo iliona ni vyema kanuni mpya zinakamilika ili kuongeza msukumo wa kutekeleza sheria ya filamu.
Alisema ili kuhakikisha kuwa kanuni zinakuwa na nguvu ya utekelezaji wa kisheria, mwaka 2009 Serikali iliunda bodi za filamu katika mikoa na wilaya, bodi hizo zitakuwa zikisamimia kanuni kwa wadau wake.
Fissoo alisema, Serikali tayari imeanzisha vyama 9 vya wadau wa filamu, ambapo alivitaja vyama hivyo ni chama cha waongozaji wa filamu, chama cha waandishi wa miswada ya filamu, chama cha watafuta mandhari.
Vyama vingine ni chama cha waigizaji, pamoja na chama cha wasambazaji filamu nchini, ambapo kati yake vyama 5 vipo hai na 4 vipo katika hatua ya uhuishaji.
Bi. Fissoo alisema ili kanuni mpya zitakelezeka vyama hivyo vitaungana na Serikali katika kuwaelimisha wanachama wao kusheshimu na kuzingatia kanuni kwani athari zilizopo katika jamii mara nyingi zimekuwa zikizalishwa na mtu mmoja mmoja.

No comments: