Napenda kuwajulisha wananchi na wadau wote kuwa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Mashirika ya Umma Sura 257 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002 (The Public Corporations Act, Cap. 257 of R.E. 2002) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Jenerali Mstaafu Robert P. Mboma kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuanzia tarehe 27 Oktoba 2011 baada ya Bodi iliyokuwepo kumaliza muda wake tarehe 26 Oktoba 2011.
Pamoja na uteuzi huo, Mheshimiwa William M. Ngeleja Waziri wa Nishati na Madini kwa Mamlaka aliyonayo amewateua wakurugenzi wanane wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania kuanzia tarehe 27 Oktoba, 2011. Walioteuliwa kuwa Wakurugenzi wa Bodi ni pamoja na:-
1. Bw. Baruany Elijah A. T. Luhanga
2. Bw. Ridhiwan Ali Masudi
3. Bw. Leonard R. Masanja
4. Bw. Vintan W. Mbiro
5. Bw. Beatus P. Segeja
6. Bw. Hassan Ally Mbaruk
7. Mhe. Victor K. Mwambalaswa (Mb.)
8. Bw. Abdul Ibrahim Kitula
Imetolewa na:
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
No comments:
Post a Comment