Thursday, October 27, 2011

Waliokufa ajali ya basi kuzikwa kaburi moja


Wananchi na polisi wakiangalia mabaki ya basi hilo baada ya kuteketea kabisa kwa moto.
Mmoja wa watu waliokuwa wakitoa mabaki ya miili ya watu walioteketea kwa moto akiendelea na zoezi la kuangalia iwapo kama kuna masalia yeyote.

Miili ya watu 12 walioteketea kwa moto katika ajali ya basi la Deluxe Coach iliyotokea Misugusugu mkoani Pwani juzi, watazikwa leo na Serikali kwa heshima zote katika kaburi moja katika eneo la Air Msae mjini Kibaha.



Eneo hilo ndipo walipozikwa watu waliopata ajali ya basi la Air Msae lililokuwa likitokea Arusha kuja Dar es Salaam miaka ya 1990.


Uamuzi huo umefikiwa na kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Pwani, iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mh. Mwantumu Mahiza kutokana na miili hiyo kuharibika vibaya na kushindwa kutambulika.


Mh. Mahiza alisema kabla ya maziko, miili ya watu hao itachukuliwa sampuli kwa ajili ya vipimo vya vinasaba (DNA) ili vifanikishe utambuzi wao.


Basi liliteketea kabisa na mabaki ya miili ya watu ililazimu kukusanywa kwa beleshi.
Picha zote na Yassin Nicas Mtei

No comments: