Tuesday, October 25, 2011

KILELE CHA WIKI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernald Membe, akipita kukagua gwaride wakati wa Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Wizara hiyo, yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo mchana.
Mbunifu wa Mitindo Fatma Amour ,akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa jijini Dar es Salaam. Fatma ni miongoni wa Wajasiriamali waliobahatika kupewa udhamini na Umoja wa Mataifa kushiriki katika wiki ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru kuonyesha bidhaa zao. (Picha na http://dewjiblog.com/
Wasanii wa Kikundi cha Tanzania House ofa Talent (THT) wakitoa burudani katika sherehe za maadhimisho hayo.
Wawakilishi kutoka Balozi mbalimbali na viongozi wa Serikali wakifuatilia sherehe hizo zilizokuwa zikendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mabalozi wastaafu nchini wakishangilia moja ya hotuba iliyosomwa katika maadhimisho ya miaka 66 ya Umoja wa Mataifa na maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo yalienda pamoja na wiki ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa kuonyesha shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na Wizara hiyo.
Wanafunzi wa shule ya Jitegemee kwa upande wa kwaya wakitoa burudani katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania na miaka 66 ya Umoja wa Mataifa.

No comments: