Friday, October 7, 2011

KILIMANJARO WASHANGILIA USHINDI WA CCM IGUNGA

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro,Vicky Nsilo Swai,akimkaribisha katibu wa CCM mkoa huo Steven Kazidi kuendelea na hotuba ya kupongeza ushindi wa chama hicho kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Igunga mkoani Tabora.
Wanachama wa CCM katika mji wa Moshi wakiwasili kwenye uwanja wa mkutano katika kata ya Kiusa mjini Moshi. Maandamano hayo yalipokelewa na mwenyekiti wa mkoa,Vicky Nsilo Swai.
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Kilimanjaro,Thomas Ngawaiya (kushoto) akipongezana na wanachama wa CCM baada ya hotuba ya mwenyekiti Swai na katibu Kazidi.

Rodrick Makundi,Moshi.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kilimanjaro kimelaani vikali tukio la kuchomwa moto gari la diwani wa kata ya Uru Kaskazini (CCM) Evarist Mumburi tukio ambalo liliambatana na kujeruhiwa vibaya kwa diwani huyo.

Tukio hilo lilitokea Septemba 2, mwaka huu muda mfupi baada ya uchaguzi wa mweneyekiti wa serikali ya kijiji cha Uru Mrawi ambao ulimpa ushindi Proti Mauki aliyepata kura 230 dhidi ya kura 207 alizopata mgombea wa Chadema.

Gari hilo lenye namba za usajili T171AFX aina ta Toyota Hilux Double Cabin,lilizingirwa na wafuasi wa Chadema waliokuwa wakipinga ushindi huo na kisha kulichoma moto na kutekeletea kabisa huku mwenyekiti wa CCM,aliyeshinda kiti hicho naye akijeruhiwa vibaya kwa kupigwa kwa mawe juu ya jicho la kulia.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kupongeza ushindi wa mgombea wa CCM katika jimbo la Igunga,Dk.Dalaly Kafumu aliyepata kura 26,484,katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro,Steven Kazidi,alisema tukio la kuchomwa moto kwa gari la diwani huyo ni unyama uliokithilika dhidi ya ubinadamu.

Kazidi alisema kuwa,tikio hilo ni mfano hai kwa chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) kwamba hakiwezi kuongoza dola na kutangaza rasmi kuwa chadema ni janga la kitaifa na wananchi wote wapenda maendeleo hawana budi kukilaani kitendo hicho.

“Chadema si chama cha kisiasa ni janga la kitaifa ni chama kinachopandikiza mbegu za chuki kwa wananchi ili waichukie serikali yao, wanapandikiza chuki vyuoni ili wanavyuo wagome,wafanye maandamano ili waichukie serikali yao”,alisema kazidi.

Katibu huyo alisema kuwa, wananchi hawana budi kutambua ya kwamba mahali popote dunia zipo changamoto na kutolea mfano wa madhehebu ya dini licha ya kuendelea kutoa mahubiri kwa jamii kuacha maovu, bado maovu yanatendeka na wanaoyatenda ni waumini wa madhehebu hayo yanayohubiri watu kuacha maovu.

Naye mweneyktii wa CCM mkoa, Vicky Nsilo Swai, alisema kuwa ushindi wa Igunga aliopata mgombea wa CCM, Dk.Dalaly Kafumu umetoa funzo kwa vyama vya upinzani kwamba wanachi wa Igunga hawadanganyiki na propaganda za kisiasa.

Akipokea mandamano makubwa yaliyohitimishwa na mkutano mkubwa wa hadhara kwenye kata ya Kiusa mjini hapa, Swai alisema kuwa, wapinzani walikuwa wakiwabeza wanaCCM kuwa watachapwa huko Igunga lakini mungu amewachapa wao.

Alisema CCM kimeshinda kihalali na kwamba hata kingezidi kwa kura moja ni ushindi na kubeza kauli za wapinzani kwamba waliibiwa kura na kuhoji mawakala wa wagombea wa vyama vya upinzani walikuwa wapi wakati wagombea wao wakiibiwa kura.

“Ushindi ni ushindi tu, hata kama ni tofauti ya kura moja tumeshinda kihalali, hatujamwagia watu tindikali, wala hatujawavua nguo wanawake”alisema mwenyekiti huyo.

Mkutano huo uliotanguliwa na maandamano yaliyoanzia kwenye ofisi za CCM mjini na kupita katika mitaa mbali mbali ya mji, ulihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa CCM katika ngazi ya mkoa.

No comments: