Waziri wa Nishati na Madini akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa kongamano la Nishati na Madini.
Baadhi ya washiriki wa kongamano la kimataifa la Nishati na Madini wakimsikiliza mtoa mada (hayupo pichani).
waziri wa Nishati na Madini akiwa kwenye moja ya mabanda ya washiriki wa kongamano la nishati na madini
waziri wa Nishati wa Madini akiwasiliza kwa makini moja ya waoneshaji wa maonesho ya nishati na madini wajulikanao kama Protea Chemicals kutoka South Afrika.
Waziri wa Nishati na Madini akizungumza na washiriki kutoka kampuni ya mafuta ya TOTAL ambao walikuwa ni moja ya washiriki wa kongamano na maonyesho ya kimataifa ya nishati na madini.
waziri wa Nishati na Madini akisalimiana na washiriki kutoka kampuni ya Geita Gold Mining.
====== ======== =======
Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William Ngeleja ameshiriki kongamano la kimataifa la nishati na madini lililofanyika tarehe 19 na 20 ) Octoba, 2011 katika hoteli ya Ngurdoto Arusha.
kongamano hilo la siku mbili limeenda sambamba na maonesho ya nishati na madini na ni la kwanza kufanyika Tanzania ambapo zaidi ya washiriki 300 kutoka nchi mbalimbali duniani wameshiriki.
katika hotuba yake Waziri wa Nishati na Madini alieleza changamoto zinazoikabili sekta za nishati na madini kama miradi mingi ya nishati na madini kuendeshwa kwa kutegemea fedha za wafadhili, kuyumba kwa uchumi kutokana na kubadilikabadilika kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na ukame.
hata hivyo alieleza kuwa Wizara inajivunia mafanikio mbalimbali ikiwemo utungwaji wa sera ya madini ya mwaka 2009 na sheria ya madini ya mwaka 2010 ambazo kwa pamoja zimewezesha Serikali kulipwa mrabaha wa asilimia nne toka asilimia Tatu kwa miaka iliyopita.
vile vile sera na sheria inaelekeza makampuni ya uchimbaji madini kutakiwa kujisajili kwenye soko la hisa ili wananchi waweze kununua na hivyo kuwa moja ya wamiliki kupitia hisa hizo.
No comments:
Post a Comment