Tuesday, October 25, 2011

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA BANDA LA MAONESHO ITU TELECOM WORLD 2011 GENEVA, SWITZERLAND


Prof. Nkoma wa TCRA akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais
alipoingia ndani ya banda la Tanzania.
Bwana Victor Nkya Akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais

Bwana Masika wa TAYOA akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais

Bwana Ahmed Habib wa Shirika la Walemavu kutoka Qatar
akimueleza Makamu wa Rais harakati za Walemavu katika kukumbukwa katika matumizi ya mawasiliano na teknolojia. Wanaoangalia baada ya Makamu ni Prof. Nkoma wa TCRA, Naibu Katibu wa ITU Bwana Houlin Zhao.

Tanzania inashiriki katika maonesho ya Teknolojia ya ITU Telecom World 2011 ambayo yameanza hapa Jijini Geneva ikiwa ni pamoja na Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la ITU. Makama wa Rais wa Tanzania Dr. Gharib Billal anahudhuria.

Tanzania inawakilishwa katika Mkutano na Maonesho haya na Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa, Viongozi mbali kutoka wizara hio, Mkurugenzi mkuu wa malmaka ya mawasiliano Tanzania, prof. John Nkoma akiambatana na watumishi wa Mamlaka hio.


Aidha Tanzania ina banda la Maonesho ambalo taasisi zifuatazo zinafanya maonesho: Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, wanaoonesha jinsi Mkongo wa Mawasiliano ulivyoIshaunganishwa na nchi zote jirani naTanzania, Wizara ya Elimu na Maendeleo ya Ufundi, wakielezea mradi mashuhuri wa Tanzania beyond Tomorrow, TAYOA, ambao wanaonesha matumizi ya teknolojia kwa ajili ya vijana katika kupambana na ukimwi pamoja na umaskini, TzNIC, ambao wanonesha matumizi na Maendeleo ya usimamizi warajisi ya .TZ kwa Watanzania badala ya matumizi ya .Com.


Makamu wa Rais, Dr. Gharib Bilal, akiongozana na Mama Zakia Bilal wametembelea Banda la Tanzania na Mabanda ya nchi za Afrika mashariki, Malawi, Ghana na Malawi.

No comments: