Monday, October 17, 2011

MAMA SALMA KIKWETE ASHIRIKI KUAGA MWILI WA MAREHEMU MAMA HAN BING JIJINI DAR LEO

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA , akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Mama Han Bing mke wa Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanya biashara wa kichina nchini Tanzania aliefariki siku kadhaa zilizopita jijini Dar es Salaam kwa kuuwawa na majambazi wasiojulikana.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,akiwa na viongozi mbali mbali kwenye ibada ya kumuombea Marehemu
Picha ya Marehemu Mama Han Bing mke wa Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanya biashara wa kichina nchini Tanzania
Kamanda wa kanda maaluum ya kipolisi ya Dar es Salaam,Suleiman Kova akiwapa pole wana jumuiya ya wachina waishio Tanzania jijini Dar es salaam wakati walipokwenda kuaga mwili wa Mama Han Bing alieuwawa na majambazi.
Wanajumuiya ya Kichina waishio nchini Tanzania wakiwa kwenye misa ya kumuombea Marehemu Mama Han Bing mke wa Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanya biashara wa kichina nchini Tanzania
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpa pole Mume wa Marehemu,Bw. Bing ambaye alikuwa ni mwenye huzuni mkubwa sana wa kuondokewa na mke wake aliyeuwawa na Majambazi siku kadhaa zilizopita.
Mama Salma Kikwete akimfariji Mtoto wa Marehemu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe akitoa salamu za pole wa wafiwa na wanajumuiya ya kichina katika msiba huo.
Mume wa Marehemu (wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na wanafamilia wengine kwenye misa ya kumuombea Marehemu.
Mmoja wa Kina Mama wa Kichina akilia kwa huzuni baada ya kuondokewa na ndugu yao.
Mmoja wa wanafamilia akimbembeleza mtoto wa Marehemu.
Picha na Mwanakombo Jumaa- Maelezo.

No comments: