Saturday, October 8, 2011

MAMA WA KICHINA AGOMA KULIPA USHURU WA MAEGESHO YA KISA JUMAMOSI SIYO SIKU YA KAZI

Moja ya watumishi wa kampuni ya AAICO ambayo ndiyo wamepewa dhamana ya kukusanya ushuru wa maegesho ya magari jijini mbeya akitoa mnyororo kulifunga gari la wachina hao huku mama wa kichina akilia kwa hasira
Mama wa kichina akimtolea maneno makali binti Eliza mkusanya ushuru wa maegesho ya magari huku mchina huyo akiendelea kugoma kuwa hawezi lipa ushuru siku ya jumamosi na jumapili kwani ni siku za mapumziko siyo siku za kukusanya ushuru
Mume wa mama mama wa kichina akijaribu nae kuwaelewesha wakusanyaji ushuru wa maegesho yamagari kuwa wameshazoea hivyo kutolipa siku ya jumamosi na jumapili kwani ni siku za mapumziko
Mama wa Kichina akiwa amechachamaa na kuelekea katika Jengo la NMB Tawi la Mbalizi Road Mjini Mbeya kuomba msaada kwa Askari Polisi waliokuwepo hapo.Picha na Mbeya Yetu Blog

No comments: