Friday, October 28, 2011

Maonyesho ya Wizara ya Fedha ya miaka 50 ya uhuru


Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Hodhi la Mali za Serikali(CHC) Dome Malosha
akipokea kikombe cha ushindi wa jumla wa kwanza wa maonyesho ya Wizara
ya Fedha ya miaka 50 ya uhuru kutoka kwa Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo jana jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Fedha Mustafa Mkulo akizindua kitabu cha historia ya Wizara ya
Fedha jana mjini Dar es salaam kwenye maonyesho ya Wizara ya Fedha ya
miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara yanayoendelea katika viwanja vya
Mnazi mmoja.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa
Dkt. Albina Chuwa akitoa ufafanuzi kwa mwananchi jana jijini Dar es
salaam wakati mwananchi huyo alipotembelea banda la Ofisi ya Taifa ya
Takwimu katika maonyesho ya Wizara ya Fedha ya miaka 50 uhuru wa
Tanzania bara.
Waziri
wa Fedha Mustafa Mkulo akisoma hotuba ya ufunguzi rasmi jana mjini Dar
es salaam maonyesho ya Wizara ya Fedha ya miaka 50 ya uhuru wa
Tanzania bara yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja.
Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar es salaam

No comments: