Friday, October 28, 2011

AJALI MBAYA IRINGA YADAIWA KUUA MMOJA


Wasamaria wema wakisaidia kumtoa dereva wa daladala baada ya ajali


Lori lililosababisha ajali eneo la Mwangata mjini Iringa mchana huu


Na francis Godwin
Dadaldala lagongana na lori katika eneo la kona za Mwangata katika manispaa ya Iringa majira ya 8 mchana na kuna taarifa kuwa mtu mmoja kufariki dunia katika ajali hiyo mbaya.
Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wameuambia mtandao huu kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Lori lenye namba za usajili T164 BDB kupita upande ambao si wake hivyo kulazimika kulivaa daladala hilo ambalo lilikuwa likishuka mteremko wa Mwangata na lori hilo likipanda mlima.
Walisema kuwa kutokana na kona hizo abiria waliokuwa katika daladala walijikuta wakikutana uso kwa uso na lori hilo.
Hata hivyo walisema zaidi ya abiria watano ndio walijeruhiwa vibaya akiwemo dereva wa daladala yenye namba T 229 BGP anayefahamika kwa jina la kazi la Kizibo.
Majeruhi wote wa ajali hiyo wamekimbizwa hospitali ya mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi huku dereva wa lori hilo amekimbia baada ya kusababisha ajali hiyo.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa (RTO) Kedmund Mnubi amethibitisha kutokea kwa ajili hiyo japo taarifa zaidi juu ya tukio hilo ameahidi kuzitoa hivi punde.

No comments: