Msanii Awilo kutoka Mbeya akiendelea kupagawisha
Msanii Ally KIba akiwasha moto katika tamasha la miaka 50 la Mtikisiko na VodaCom Iringa ,Ruvuma na Mbeya.
Mratibu wa tamasha la miaka 50 ya uhuru la Mtikisiko na Vodacom Edwin Bashir akiwa katika jukwaa.
MR Bluu akiwasha moto ndani ya ukumbi wa Ebony Shimoni Mafinga. |
Dj Emani Kwasa akiwa na mtangazaji Bony Zacharia wa radio Ebony FM katika jukwaa. |
Na Francis Godwin
Matamasha ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika maarufu kwa jina la Mtikisiko na Voda Com na Pepsi yanayoendelea katika mikoa ya nyanda za juu kusini kwa maana ya Iringa ,Ruvuma na Mbeya yamezidi kuacha historia iliyofichika katika mikoa hiyo kwa wapenda burudani.
Matamasha haya ya miaka 50 ya uhuru Mtikisiko na Voda Com na Pepsi ambayo tayari yamepata kuacha simulizi katika mji wa Ilula wilaya ya Kilolo na mji wa Mafinga wilaya ya Mufindi hivi sasa mashambulizi zaidi yanaelekea katika mji wa Makambako wilaya ya Njombe mkoa mpya wa Njombe ambako burudani itawashukia wakazi wa Makambako siku ya jumamosi kwenye viwanja vya Amani na jumapili wakazi wa mji wa Songea kutekwa ndani ya uwanja wa Maji maji .
Katika mji wa Mafinga mashabiki wa burudani waliopata kukutana uso kwa uso na wasanii Ally Kiba ,MR.Bluu na wasanii maarufu kutoka mkoa wa Iringa Nemo pamoja na Awilo kutoka mkoa wa Mbeya ,wamepata kukishukuru kituo cha radio Ebony Fm kwa kuonyesha njia katika burudani mikoa ya nyanda za juu kusini na kuwa matamasha kama hayo hayajapata kutokea na kuomba yazidi kuendela zaidi na zaidi.
Mwenyekiti wa watuma salamu mkoa wa Iringa Dkt Said Utenga aliwashukuru waandaaji wa matamasha hayo ya miaka 50 ya uhuru Mtikisiko kilaru laru na Voda Com 2011 alisema kuwa hatua hiyo ni kubwa na inapaswa kupongezwa na wananchi na viongozi pia wa mikoa husika.
Kwani alisema kuwa vipo vitu vingi vya radio ila kazi inayofanywa na radio Ebony Fm katika kuenzi miaka 50 ya uhuru kwa kuwakutanisha wananchi katika burudani ya pamoja ni jambo jema ambalo linapaswa kuungwa mkono.
Hata hivyo pamoja na mkusanyiko mkubwa wa wapenda burudani kujitokeza katika uwanja wa RMA Mafinga kupata burudani halisi bado umati mkubwa zaidi ulipata kujitokeza katika ukumbi wa Ebony Shimoni mafinga ambako hadi majira ya saa 8 usiku nusu ya wapenda burudani walikuwa katika foleni nje ya ukumbi wakitaka kuingia katika ukumbi huo ambao hata hivyo ulionekana kujaza zaidi kabla ya vyombo vya usalama kuwazuia kuendelea kuingia ndani ya ukumbi huo .
Kazi nzuri iliyofanywa na askari polisi chini ya afande Ghatto Mfaume na mkuu wa polisi wilaya ya Mufindi (OCD) Kakamba ya kuzuia mashabiki hao kuendelea kuingia katika ukumbi huo iliweza kusaidia kuondoa lawama kwa mashabiki hao ambao waliona kama waandaaji wa tamasha hilo na kuwa kama wanawanyima kuungana na wenzao ndani ya ukumbi kupata burudani zaidi.
Tayari mratibu wa tamasha hilo Bony Zacharia amepata kuwashukuru wadau wa burudani mjini Mafinga kwa kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo na kuwaomba radhi wale ambao walishindwa kuingia ukumbini kutokana na ukumbi kujaa zaidi.
Huku akiwataka wakazi wa mji wa Makambako ,Njombe ,Songea na Chimala na Mbeya kujindaa kwa burudani kama hiyo .
No comments:
Post a Comment