Thursday, October 6, 2011

MITIHANI YA TIFA KWA KIDATO CHA PILI YA RUDI, WALIOKOSA ELIMU YA SEKONDARI + CHUNYA + MBEYA KUSOMA BURE


Naibu Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Tanzania Philipo Mulugo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Songwe lililopo wilayani Chunya mkoani Mbeya aliyesimama akitoa hotuba katika moja ya mikutano yake.

Na mwandishi wetu.
Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi mheshimiwa Philipo Mulugo amesema serikali imerejesha mtihani wa taifa wa kidato cha pili ili kupunguza kushuka viwango vya ufaulu hasa kwa kidato cha nne nchini.

Ameyasema hayo wakali alipokuwa akiwahutubia wananchi waliompa dhamana ya ubunge katika jimbo la Songwe, wilaya ya Chunya mkoani Mbeya na kuongeza kuwa wastani wa ufaulu wa mtihani huo utakuwa ni alama 25.


Amesisitiza kwa kusema kwamba kuanzia mwaka huu hakuna mwanafunzi ambaye ataruhusiwa kuendelea na masomo ya kidato cha tatu kama hatukuwa amefanya mtihani wa kidato cha pili na kupata alama zilizowekwa.


Taarifa tulizozipata zinadai kuwa wanafunzi ambao wamekuwa wakifanya vibaya katika mitihani yao ya kidato cha nne ndio hao ambao wamekuwa wakifanya vibaya katika mitiyani yao ya kidato cha pili
Wakati huo huo mheshimiwa Mulugo amesema wananchi waliokosa elimu ya Sekondari wametangaziwa neema ya kusoma bure elimu ya Sekondari Jimboni humo.


Mulugo alisema kuwa kwa kuanzia tayari anasomesha wananchi 20 jambo ambalo alisema kuwa linamuumiza kwani yupo tayari kuwalipia wananchi wote wenye uhitaji wa elimu hiyo ya Sekondari ambapo anatarajia kuanzisha Maktaba ya Jimbo ambayo itakuwa eneo la Mkwajuni.

Alisema kuwa Jimbo hilo la Songwe na wilaya nzima ya Chunya ni moja ya wilaya ambazo zipo nyuma sana kielimu jambo ambalo viongozi wanaopata fursa akiwemo yeye ni lazima wafanya jitihada za kuwasaidia wenye uhitaji.

Naibu Waziri huyo wa elimu maarufu kama Mulugo Ahadi umepata, aliongeza kuwa kufikia mwakani 2012 atafarijika endapo wananchi hao watajitokeza kujiunga na vituo hivyo vinavyotoa mafunzo ya elimu ya Sekondari kwasababu ulimwengu uliopo sasa unahitaji wasomi ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoukabili.

No comments: