Saturday, October 22, 2011

MWENYEKITI WA WAMA MAMA SALMA KIKWETE AKUTANA NA UJUMBE WA MASUALA YA AFYA KUTOKA MAREKANI.




Katibu wa Taasisi ya WAMA Daudi Nasibu (aliyesimama) akitoa taarifa kwa wageni wanaoshughulikia mambo ya afya kutoka Marekani pamoja na uongozi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii nchini 0kt-20-2011 katika Ofisi za WAMA walipokutana na Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mama Salma Kikwete kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusu kusaidia kuleta vifaa tiba kwaajili ya jitihada za kupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga nchini.




Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Zakhia Meghji (kulia) akibadilishana mawazo katika ofisi za WAMA jijini Dar es Salaam Oktoba 20,2011 na wajumbe kutoka Marekani wa taasisi inayotambulika kama GE healthymagination inayoshughulikia mambo ya huduma za afya ( kushoto) ni Mkurugezi wa Global Programs healthymogination Joneen UzzelI na (aliesimama katikati) ni Mkurugenzi mwenza wa mpango wa ushirikiano wa wake wa Marais wa nchi za Afrika (( Co- Director of African First Ladies Fellowship Program) Cora Neumann, wakati ujumbe huo ulipokwenda kumtembelea Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (hayupo pichani ) na kuzungumzia jinsi ya kusaidia kuleta vifaa tiba kwa ajili ya kusaidia kupunguza vifo vya akinamama na watoto wachanga nchini .




Katibu wa Taasisi ya WAMA Daudi Nasibu (kulia) akiagana na Mjumbe kutoka Marekani wa Taasisi hiyo(kushoto) Reza Bundy baada ya kumaliza mazumgumzo na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete, (pichani hayupo) Mazungumzo hayo pia yamewahusisha wataalamu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Blandina Nyoni hayupo pichani – Oktoba 20-2011.





Picha ya pamoja baada ya Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete kumaliza mazungumzo na ujumbe wa masuala ya afya kutoka Marekani pamoja na uongozi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. (Picha na Mwanakombo Jumaa-Oktoka 20.2011 Dar es Salaam).

No comments: