Habari marafiki, leo nina furaha isiyo kifani kwa kuweza kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa ** **25 Yrs**** hakika Mungu ni mkuu nawashukuru nyote kwa kushirikiana nami bega kwa bega katika kipindi chote cha maisha yangu nawatakia kila lakheri..
Mnamo October 21,1985, Kwa upando niliweza kuzaliwa ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Ilala Dar es Salaam,Tanzania najivunia kua mtanzania ila ndani ya miaka hii yote 25 nakumbuka mengi na nimepitia mengi ikiwemo milima na mabonde machozi na jasho la damu.
Kwa kifupiu, mpaka kufikia leo Oct 21, nafikisha miaka 25, kamili, lakini hapo hapo natimiza miaka 12 ya mateso katika hai ya kuishi pekee yangu (kujitegemea) ni hakika naeleza nimepitia mateso makubwa huku kubwa kuliko ni la kuishi katika maisha ya mtoto wa mitaani (Street children) lakini Mungu alikua nami na wasamalia wema wakanitoa huko na sasa nipo hapa nilipo.
Hivyo kwa mateso niliyopitia kwa zaidi ya miaka hiyo 12, na leo kutimiza miaka 25 ni faraja sana kwangu na namshukuru Mungu kwani bado yupo na mimi siku zote na hakika matunmda yake nayaona mbali ya kuwa na vikwazo vingi mbele yangu.
Hivyo basi leo nawashukuru nyote kwa kua nami bega kwa beka kwa kipindi hiki na kijacho shukrani ziwafikie wote wakiwemo kwa uchache Bosi wangu, Ablsolum Kibanda (Freemedia Ltd), Mohamed Dewji (MB-Singida mjini), famlia ya Mnyanga,Simtoe,Mtweve,Munaar,Wafanyakazi wote wa Freemedia Ltd * Tanzania Daima na Sayari, wafanyakazi wenzangu na wanachama wa kikosi cha maafa na uokoaji Tanzania Red cross, Shyrose Bhanji, Agustine Chale(baba mkubwa) Living Faith Church, familia ya Monga, wanafunzi wote Gilman Ruthinda primary LY 2002,wanafunzi sekondar-Mbalizi High na Meridian High ..bila kuwasahau wanafunzi wa Royal Collage of Tanzania, Red Cross Tanzania First Aids Collage na wengine wengi nyote nawashukuru sana I say Igweeeeeeeee....and Blogger nyote Igweeeeeee....asante
Mwisho
No comments:
Post a Comment