Sunday, October 2, 2011

Rais Kikwete amfariji Professa Ndulu kwa kufiwa na mama yake mzazi

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mama wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Professa Beno Ndulu kufuatia kifo cha mama yake mzazi Bibi.Regina Steven Mpangile kilichotokea juzi(30/9/2011) katika hospitali ya Hubert Kairuki jijini Dar es Salaam.Kushoto aliyesimama ni Professa Beno Ndulu.Marehemu Regina anatarajiwa kuzikwa kesho katika makaburi ya Kinondoni. Rais Kikwete alikwenda nyumbani kwa marehemu ,Tabata jijini Dar es Salaam kutoa pole na kuifariji familia ya marehemu.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Gavana wa Benki Kuu Professa Beno Ndulu wakiwafariji ndugu na jamaa wa mama wa Gavana Marehemu Bibi.Regina Steven Mpangile nyumbani kwa marehemu Tabata jijini Dar es Salaam leo jioni.Maremu Bibi Regina alifariki juzi katika Hospitali ya Hubert Kairuki jijini Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa kesho(jumatatu) katika makaburi ya Kinondoni.
Picha na Freddy Maro wa Ikulu

No comments: