Wednesday, October 12, 2011

Rais Kikwete ashiriki katika mazishi ya Harith Mwapachu,mtoto wa kiume wa Katibu mkuu mstaafu wa jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Juma Mwapachu



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la marehemu Harith Juma Mwapachu aliyefariki jana asubuhi na kuzikwa leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo mchana.Kulia nia Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal ambaye pia alishiriki mazishi hayo.Marehemu Harith ni mtoto wa kiume wa Balozi Juma Mwapachu katibu mkuu mstaafu wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(watatu kushoto),Balozi Juma Mwapachu(kushoto), Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal(wapili kushoto), Rais Mstaafu awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi,(wanne kushoto) na Waziri Mstaafu Bakari Mwapachu(kulia)wakiwa katika swala ya kumuombea Marehemu Harith Juma Mwapachu wakati wa mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo mchana.Marehemu Harith aliyefariki jana asubuhi ni Mtoto wa kiume wa balozi Juma mwapachu .

(picha na Freddy Maro).

No comments: