Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni ndugu Hermas Mwansoko akifungua Mwenge wa kwanza wa Uhuru uliowashwa tarehe 9 Disemba 1961 kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro ,ambao kwa kiasi kikubwa uliiga falfasa za mwenge uliokuwa ukitumiwa na kabila la Wazanaki. Sherehe hizo zilifanyika katika makumbusho ya Baba wa Taifa, kijiji Butiama, mkoani Mara.
Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni, ndugu Hermas Mwansoko (kulia) akishika mwenge wa Uhuru wa kwanza baada ya kuuzindua rasmi kwenye makumbusho ya Baba wa taifa, Hayati Mwalimu Nyerere leo (jana) kijijini kwake Butiama. Aliyeshika wa pili kushoto ni Chifu Japhet Wanzagi ambaye ni ndugu katika ukoo wa Hayati Mwalimu Nyerere, wa kwanza kushoto ni mtoto wa Mwalimu, Madaraka Nyerere akishuhudia tukio hilo.
Picha Na Anna Itenda - Maelezo
No comments:
Post a Comment