Tuesday, October 18, 2011

Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein Azindua Matayarisho ya Kilimo Cha Mpunga Kwa Msimu Wa Mwaka 2011-2012

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na wakulima wa bonde la mpunga la Cheju Wilaya ya Kati Unguja, baada ya kuzindua matayarisho ya kilimo cha Mpunga kwa msimu wa mwaka 2011-2012,katika Mkoa wa kusini Unguja
Mwakilishi wa Jumuiya za wakulima katika bonde la cheju Getruda Adolfi Mkude,akisoma risala ya wakulima katika uzinduzi wa kilimo cha mpunga kwa msimu huu wa mwaka 2011-2012,ambapo wastani wa ekari elfu tatu zitalimwa mpunga kwa kutumia mbegu za kisasa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akiwasalimia viongozi wa jumuiya za wakulima katika bonde la cheju alipowasili kuzindua kilimo hicho kwa msimu wa mwaka 2011-2012,katika bonde la mpunga la Cheju Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja
Wakulima waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa kilimo cha mpunga kwa msimu wa mwaka 2011-2012,katika bonde la Cheju Wilaya ya kati Mkoa wa kusini Unguja,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wakulima hao naa kuwataka kutumia mbegu bora za kisasa ili kukuza pato katika kilimo hicho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akiwasha Trekta kama ishara ya uzinduzi wa kilimo cha Mpunga kwa msimu wa mwaka 2011-2012,katika bonde la mpunga la Cheju Wilaya ya katika Mkoa wa kusini Unguja
Baadhi ya matrekta yakianza kuchimbua katika hatua za matayaarisho ya kilimo cha mpunga katika bonde la Cheju, kwa mwaka 2011-2012 kilichozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,jana katika bonde hilo Wilaya ya kati Unguja
Baadhi ya matrekta yaliyotayarisha katika kazi ya kuburuga katika matayarisho ya kilimo cha mpunga katika Bonde la mpunga la Cheju,Wilaya ya Kati Unguja kwa msimu wa 2011-2012.Picha na Ramadhan Othman, Ikulu-Zanzibar



No comments: