Saturday, October 29, 2011

Rais wa Zanzibar Dr Shein azindua boti mpya ya Azam marine.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa Boti Mpya ya Kilimanjaro 111, inayomilikiwa na kampuni ya usafiri wa Baharini (Azam Marine) inayomilikiwa na Nd.Salim Said Baghresa,(wa pili kulia) ambayo hufanya safari zake kutoka Zanzibar- Dar es Salaam, na uwezo wa kuchukua abiria 540 kwa wakati mmoja,uzinduzi huo ulifanyika leo katika bandari ya Malindi Zanzibar,(kushoto) ni Waziri wa Miundimbinu na Mawasiliano Masoud Hamad Masoud,(Kulia) ni Baharia Kassim Siri Matola
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa nahodha wa Kilimanjaro111,Clement R.Mgalula,wakati alipotembelea chumba cha nahodha huyo ambako shuhuli za uendeshaji wa chombo hicho hufanyika,baada ya uzinduzi rasmi,(wa tatu kushoto)mmiliki wa kampuni ya usafiri wa Baharini Azam Marine Nd.Salim Said Baghresa,ambayo hufanya safari zake kutoka Zanzibar- Dar es Salaam,uzinduzi huo ulifanyika leo katika bandari ya Malindi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Nahodha wa Boti ya Kilimanjaro 111,Clement R.Mgalula,jinsi ya kuaza kuiondosha boti ikiwa imefunga gati, katika Bandari ya Malindi na kuanza kuondoka kufanya safari zake, kutoka Zanzibar- Dar es Salaam,uzinduzi huo ulifanyika leo katika bandari ya Malindi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za uzinduzi wa Boti Mpya ya Kilimanjaro111,inayomilikiwa na kampuni ya Usafiri wa Baharini ya Azam Marine ,inayo safiri kutoka Zanzibar-Dar es Salaam,ikiwa na uwezo wa kuchukua abiria 540 kwa wakati mmoja,(kulia) Nd.Salim Said Baghresa,na (kushoto) ni Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Masoud Hamad Masoud,uzinduzi huo ulifanyika leo katika bandari ya Malindi Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akipokea zawadi kutoka kwa mmiliki wa kampuni ya usafiri wa Baharini (Azam Marine) Nd.Salim Said Baghresa,wakati wa uzinduzi wa Boti mpya ya Kilimanjaro111,ambayo hufanya safari zake kutoka Zanzibar- Dar es Salaam,uzinduzi huo ulifanyika leo katika bandari ya Malindi Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa mmiliki wa kampuni ya usafiri wa Baharini (Azam Marine) Nd.Salim Said Baghresa,wakilekea katika Boti ya Kilimanjaro111 kufanya uzinduzi rasmi wa Boti hiyo,ambayo hufanya safari zake kutoka Zanzibar- Dar es Salaam,ikiwa na uwezo wa kuchukua abiria 540,kwa wakati mmjoa,uzinduzi huo ulifanyika leo katika bandari ya Malindi Zanzibar,(kushoto) Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Hamad Masoud Hamad.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na mmiliki wa kampuni ya usafiri wa Baharini Azam Marine Nd.Salim Said Baghresa,wakati wa uzinduzi wa Boti mpya ya Kilimanjaro111,ambayo hufanya safari zake kutoka Zanzibar- Dar es Salaam,uzinduzi huo ulifanyika leo katika bandari ya Malindi Zanzibar,(katikati) Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Masoud Hamad Masoud
Baadhi ya waalikwa katika hafla ua uzinduzi wa Boti Mpya ya Kampuni ya Azam Marine,Kilimanjaro111,wakiwa katika sherehe hizo zilizofanyika katika viwanja vya Bandarini Malindi Zanzibar,ambapo uzinduzi wa boti hiyo ulifanywa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Aliu Mohamed Shein,(hayupo pichani).Picha na Ramadhan Othman Ikulu Zanzibar.

No comments: