Sunday, October 30, 2011

Happy Birthday 8020 Blog kutimiza miaka 5



Mgeni Rasmi katika hafla ya kutimiza miaka 5 ya 8020 Fashions Blog, Mbunge wa Viti Maalum wa CCM,Mh. Angelah Kairuki akisoma hotuba fupi ya ufunguzi wa hafla hiyo iliyofanyika mchana wa leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee V.I.P Hall jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi na Mmiliki wa Blog ya 8020 Fashions,Shamim Mwasha a.k.a Zeze akizungumza wakati wa hafla hiyo ambayo ilihudhuliwa na wadau mbali mbali na kufana sana.
Mc wa Shughuli hiyo,Dina Marios (kulia) akizungumza na Da' Shamim Mwasha wakati wa hafla hiyo iliyofana sana na kupendeza.
Wadau Mbali Mbali walijitokeza kumpa tafu Da' Shamim Mwasha katika hafla ya Besdei ya kuzaliwa kw Libeneke lake la 8020 Fashions Blog kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee V.I.P Hall,jijini Dar
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Mbunge wa Viti Maalum wa CCM,Mh. Angelah Kairuki akimlisha kipande cha keki Da' Shamim Mwasha.
Mrs. Ankal (kulia) akimlisha kipande cha keki Da' Shamim,huku Mh. Angelah Kairuki akishuhudia.Keki hiyo ni zawadi maalum kutoka kwa Ankal Michuzi a.k.a Mzee wa Libeneke.
Da' Mwamvita Makamba (pili shoto),Da' Mwammy Mlangwa (pili kulia) wakiwa na wadau wengune wa Vodacom Tanzania.


No comments: