Vituo vitakavyouza tiketi hizo hadi saa 10 jioni ni Uwanja wa Taifa, kituo cha mafuta cha Oilcom Ubungo, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, kituo cha mafuta cha Big Bon kilichoko Msimbazi- Kariakoo na mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Samora/Ohio.
Pia tiketi zitauzwa siku ya mchezo katika magari maalumu yatakayoegeshwa katika maeneo ya uwanja.
Tunatoa mwito kwa mashabiki kununua tiketi zao mapema ili kuepuka bughudha ya kuingia uwanjani siku ya mechi.
Viingilio katika pambano hilo ni sh. 5,000 kwa viti vya kijani na bluu (tiketi 36,000), sh. 7,000 viti vya rangi ya chungwa (tiketi 11,000) sh. 10,000 VIP C (tiketi 4,000), sh. 15,000 VIP B (tiketi 4,000) na sh. 20,000 VIP A (tiketi 700).
Waamuzi wa mechi hiyo ni Oden Mbaga (centre referee), Hamis Chang’walu (assistant 1) na John Kanyenye (assistant 2). Mtathimini wa waamuzi (referee assessor) ni Soud Abdi wakati kamishna wa mchezo huo ni Mohamed Nyange.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment