Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Barnabas amekutwa amejinyonga hadi kufa alfajiri ya leo nyumbani kwake,taarifa zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo ambapo Camera ya JIACHIE ilifika kupata tukio, wameeleza kuwa Marehemu alikuwa na ugomvi wa muda mrefu na Mkewe,hivyo usiku wa kuamkia leo,ilitokea kufarakana kwa kaisi kikubwa na kupelekea mkewe Merehemu kuondoka usiku wa Manane akiwa na mtoto wake mdogo.Pichani ni askari wa kituo cha Kawe wakiupakiza mwili wa Marehemu Barnabas kwenye gari ya polisi kwa uchunguzi zaidi.
Mwili wa Marehemu Baranabas ukitolewa nje na askari wa kituo cha kawe huku umati mkubwa wa watu ukilishuhudia tukio hilo la kuhudhunisha.
Marehemu Barnabas akining'inia mara baada ya kujinyonga na kitambaa mapema leo asubuhi nyumbani kwake.
Mwili wa Marehemu ukitolewa nje na askari kwa ajili ya kupelekwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi.
Ndugu wa Marehemu pamoja na Mwenyikiti wa serikali ya Mtaa wa Kawe wakizungumza kwa ufupi kuhusiana na tukio hilo mbele ya Camera ya Clouds TV,ambalo limezua huzuni kubwa miongoni mwa baadhi ya wakazi wa Kawe,Kinondoni jijini Dar.
Umati wa wakazi wa kawe waliofika kulishuhudia tukio hilo la kusikitisha,lilitokea alfajiri ya leo,Kawe-Ukwamani,Kinondoni jijini Dar.Mungu akailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi-Amin.
Habari kwa Hisani ya Jiachie Blog
No comments:
Post a Comment