NA Francis Godwin
KAMATI ya kituo cha afya Mbuyuni Wilayani Chunya Mkoani Mbeya Imepinga malipo ya mzabuni wa ukarabati wa kituo hicho kutokana na ufisadi uliofanywa na watendaji wa halmshauri hiyo kwa kutokuwa na maelezo ya fedha zaidi sh.mil.10.
Mwandishi wa mtandao huu kutoka Mbeya Esther Macha anaripoti kuwa ,Ufisadi uliobainika kufanyika katika Kituo cha Afya Mbuyuni ni pamoja na wizi wa fedha za mradi pamoja na udanganyifu katika utekelezaji wa mradi huo ambapo kiasi ghicho cha fedha hakina maelezo kutokana na watendaji hao kupishana kauli.
Pamoja na udanganyifu huo pia kazi hiyo ilifanyika chini ya kiwango lakini mzabuni akalipwa fedha kwa kazi hiyo. Kamati ya Kituo hicho ilitoa madai ya kuwepo wizi wa vifaa vya ukarabati uliokuwa ukifanywa na mafundi lakini mzabuni alipuuza .
Wakizunguza katika kikao na Naibu waziri wa elimu na mafunzo Bw.philipo Mulugo,uongozi wa kituo hicho ulianza kulalamikia mradi huo kuanzia Juni mwaka 2009 lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
Wauguzi hao walisema kuwa pamoja na Kamati yake kuwasilisha malalamiko yao kwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Bw. Philip Mulugo.
Hata hivyo Bw.Mulugo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songwe kiliko kituo hicho alilazimika kukutanisha uongozi wa halmashauiri na uongozi wa kituo na kamati ya ujenzi katika kikao hicho ambapo zaidiya sh. Mil.zilikosa maelezo kutokana na viongozi hao kujichanya katuika kutoa taarifa hiyo ya matumizi.
Akizungumzia sakata hilo katika kikao hicho ambacho kilifanyika katika Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Bw.Maurice Sepanjo pamoja na Mkuu wa Kituo hicho cha Afya, wote wanabainisha kuwa awali mradi huo ulitengewa sh. Mil.52, hata hivyo mkanganyiko unajitokeza kwenye matumizi ya fedha hizo pamoja na ukweli wa kazi iliyofanyika.
Ukarabati wa Kituo cha Afya Mbuyuni kilichopo tarafa ya Songwe wilayani Chunya ulianza Apili nne mwaka 2008 na ulitarajiwa kukamilika Juni 29 mwaka huo huo wa 2008.
Mkandarasi aliyeshinda zabuni hiyo ametajwa kwa jina la Bw. Masha Benard wa Chunya, hata hivyo tangu akabidhiwe kazi amekuwa akisuasua na hadi leo hajakamilisha na hata hiyo kazi alokwishaitekeleza kidogo inaelezwa kuwa chini ya kiwango huku taarifa za fedha zikionyesha kwamba zimetumika zote.
Kwa mujibu wa taarifa ya uongozi wa Kituo hicho kazi ambazo hazijatekelezwa ni pamoja na ukarabati wa mfumo wa maji safi na maji taka, ukarabati wa jiko, ukarabati wa vitanda, ununuzi wa samani na vitendea kazi na umaliziaji kazi ambazo hazikukamilika.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kituo hicho,Bw. Bruno Mbegeze (69) anabainisha kufanyika kwa udanganyifu katika utekelezaji wa mradi huo ikiwemo malipo na kazi yenyewe na kwamba walilazimishwa kusaini muhtasari wa kuidhinisha malipo huku kiwango cha fedha kikiwa hakijaonyeshwa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment